The chat will start when you send the first message.
1Wafilisti walipopigana na Waisiraeli, watu wa Waisiraeli wakawakimbia Wafilisti kwa madonda waliyopigwa, wakaanguka wakafa kule mlimani kwa Gilboa.
2Wafilisti wakawafuata na kuandamana na Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua wana wa Sauli: Yonatani na Abinadabu na Malkisua.
3Mapigano yakawa makali hapo, Sauli alipokuwa; wapiga mishale walipomwona, akaumizwa sana nao wapiga mishale.
4Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichoma na kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.[#Amu. 9:54.]
5Mchukua mata yake alipoona, ya kuwa Sauli amekufa, naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.
6Ndivyo, Sauli alivyokufa na wanawe watatu na mchukua mata yake na watu wake wote, wote pia siku hiyohiyo.
7Watu wa Waisiraeli waliokaa ng'ambo ya huko ya hilo bonde na ng'ambo ya huko ya Yordani walipoona, ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia nao; kisha Wafilisti wakaja, wakakaa humo.
8Ikawa kesho yake, Wafilisti walipokuja kuwapambua waliouawa wakamwona Sauli na wanawe watatu, jinsi walivyokufa mlimani kwa Gilboa.
9Wakamkata kichwa, wakampambua mata yake, wakatuma wajumbe kwenda po pote katika nchi ya Wafilisti na kuyatangaza penye nyumba ya vinyago vyao, hata kwa watu.
10Mata yake wakayaweka nyumbani mwa Maastaroti, nao mzoga wake wakautungika bomani kwa mji wa Beti-Sani.
11Wenyeji wa Yabesi wa Gileadi walipoyasikia, Wafilisti waliyomfanyizia Sauli,[#1 Sam. 11:1-11.]
12Wakaondoka watu wote walioweza kupiga vita, wakaenda usiku wote, wakauchukua mzoga wa Sauli, nayo mizoga ya wanawe pale bomani kwa Beti-Sani, kisha wakarudi na kuipeleka Yabesi, wakaiteketeza huko kwa moto.
13Kisha wakaichukua mifupa yao, wakaizika chini ya miombo kwao Yabesi, wakafunga mfungo siku saba.[#2 Sam. 1:12.]