The chat will start when you send the first message.
1Kazi zote, ambazo Salomo aliifanyia nyumba ya Bwana zilipomalizika, Salomo akavipeleka vipaji vitakatifu vyote vya baba yake Dawidi pamoja na fedha na dhahabu na vyombo vyote, akaviweka penye vilimbiko vya nyumba ya Mungu.[#1 Mambo 28:14-18.]
2Kisha Salomo akawakusanya wazee wa Waisiraeli nao wote waliokuwa vichwa vya mashina nao wakuu wa milango ya wana wa Isiraeli mle Yerusalemu kwenda kulitoa Sanduku la Agano la Bwana katika mji wa Dawidi ulioitwa Sioni.
3Ndipo, watu wote wa Isiraeli walipkusanyika kwa mfalme kufanya sikukuu, ikawa mwezi wa saba.[#3 Mose 23:34.]
4Wazee wote wa Isiraeli walipokwisha fika, Walawi wakalichukua hilo Sanduku.
5Wakalipeleka Sanduku pamoja na Hema la Mkutano na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa Hemani, hivyo watambikaji walio Walawi wakavipandisha.
6Naye mfalme Salomo pamoja na mkutano wote wa Waisiraeli waliokusanyika kwake mbele ya hilo Sanduku wakatoa mbuzi na kondoo na ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko, nao hawakuhesabika, wala hawakuwangika kwa kuwa wengi mno.
7Watambikaji wakaliingiza Sanduku la Agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani kiitwacho Patakatifu Penyewe, wakaliweka chini ya mabawa ya Makerubi.
8Yale Makerubi yalikuwa yameyakunjua mabawa juu ya mahali pale, Sanduku lilipowekwa; ndivyo, Makerubi yalivyolifunika juu hilo Sanduku nayo mipiko yake.
9Kwa urefu wa mipiko pembe zao hii mipiko zikaoneka kutoka penye Sanduku kuelekea mle chumbani mwa ndani, lakini nje hazikuoneka; nayo imo humo mpaka siku hii ya leo.
10Mle Sandukuni hamkuwamo na kitu, ni zile mbao mbili tu, Mose alizozitia huko Horebu, Bwana alipofanya Agano na wana wa Isiraeli, walipotoka Misri.[#Ebr. 9:4.]
11Kisha watambikaji wakatoka Patakatifu; nao hawa watambikaji waliooneka hapo walikuwa wamejitakasa wote pasipo kuziangalia zamu zao,
12nao waimbaji wote pia walio Walawi, wale wa Asafu na wa Hemani na wa Yedutuni pamoja na wana wao na ndugu zao, wote walikuwa wamevaa nguo za bafta, wakashika patu na mapango na mazeze, wakawa wamesimama upande wa maawioni kwa jua penye meza ya kutambikia, tena walikuwako pamoja na watambikaji 120 wenye kupiga matarumbeta.[#1 Mambo 15:19; 16:37,41-42; 25:1-7.]
13Palipotukia pa kupigia matarumbeta na kuimba nyimbo, ikawapasa wote kuzisikiza sauti zao kwa mara moja kuwa kama mtu mmoja tu, wamshangilie Bwana na kumshukuru wakipaza sauti na kupiga matarumbeta na patu na vyombo vyote vya kuimbia, wamshangilie Bwana, ya kuwa ni mwema, ya kuwa upole wake ni wa kale na kale. Ndipo, Nyumbani mlipojaa wingu, humo Nyumbani mwa Bwana.[#1 Mambo 16:34.]
14Nao watambikaji hawakuweza kusimama humo na kuzifanya kazi za utumishi wao kwa ajili ya hilo wingu, kwani utukufu wa Bwana uliijaza Nyumba ya Mungu.[#2 Mambo 7:1,3.]