The chat will start when you send the first message.
1Hizo siku zake Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, akapanda huko; ndipo, Yoyakimu alipomtumikia miaka 3, kisha akamkataa tena akiacha kumtii.
2Ndipo, Bwana alipotuma kwake vikosi vya Wakasidi na vikosi vya Washami na vikosi vya Wamoabu na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma katika nchi ya Yuda, waiangamize kwa lile neno la Bwana, alilolisema vinywani mwa watumishi wake wafumbuaji.
3Hivyo vikaingia katika nchi ya Yuda kwa lile neno, kinywa cha Bwana kililolisema, aiondoe usoni pake kwa ajili ya makosa ya Manase, aliyoyafanya yote.[#2 Fal. 21:10-16; 23:26-27.]
4Hata kwa ajili ya damu zao wasiokosa, alizozimwaga, akaujaza Yerusalemu hizo damu zao wasiokosa, kwa sababu hii Bwana hakutaka kuwaondolea makosa.
5Mambo mengine ya Yoyakimu nayo yote, aliyoyafanya, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
6Yoyakimu alipokwenda kulala na baba zake, mwanawe Yoyakini akawa mfalme mahali pake.
7Lakini mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwani mfalme wa Babeli aliichukua nchi yote iliyokuwa yake mfalme wa Misri toka kwenye mto wa Misri mpaka kwenye jito la Furati.
8Yoyakini alikuwa mwenye miaka 18 alipoupata ufalme, akawa mfalme miezi 3 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Nehusta, binti Elnatani, wa Yerusalemu.
9Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, baba zake waliyoyafanya.[#2 Fal. 23:37.]
10Wakati huo wakapanda watumishi wa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, kwenda Yerusalemu, mji huu ukaja kusongwa kwa kuzingwa.
11Naye Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, akaja Yerusalemu, watumishi wake walipokuwa wakiusonga huo mji kwa kuuzinga.
12Ndipo, Yoyakini, mfalme wa Wayuda, alipomtokea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake na watumishi wake na wakuu wake na watumishi wake wa nyumbani, naye mfalme wa Babeli akamchukua katika mwaka wa 8 wa ufalme wake yeye.
13Akatoa navyo vilimbiko vyote vya Nyumba ya Bwana na vilimbiko vya nyumba ya mfalme, dhahabu na vyombo vyote, Salomo, mfalme wa Waisiraeli, alivyovitengeneza vya kutumiwa Jumbani mwa Bwana, akavivunjavunja, kama Bwana alivyosema.[#2 Fal. 20:17.]
14Akawahamisha Wayerusalemu wote na wakuu wote na mafundi wa vita wenye nguvu, nao walikuwa mateka 10000 na mafundi wote na wahunzi, hakusalia mtu, wasipokuwa watu wanyonge wa nchi hiyo.
15Naye Yoyakini akamhamisha kwenda Babeli na mamake mfalme na wakeze mfalme na watumishi wake wa nyumbani, nao wenye macheo katika nchi hii akawatoa Yerusalemu na kuwapeleka Babeli kifungoni.[#2 Fal. 25:27; Yer. 22:26; 24:1.]
16Tena wenye nguvu wote 7000, na mafundi na wahunzi 1000, wote ni mafundi wa kweli wa kupiga vita; hao mfalme wa Babeli akawapeleka Babeli kifungoni.
17Kisha mfalme wa Babeli akamfanya baba yake mdogo Matania kuwa mfalme mahali pake, akaligeuza jina lake, akamwita Sedekia.
18Sedekia alikuwa mwenye miaka 21 alipoupata ufalme; akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu; jina la mama yake ni Hamutali, binti Yeremia, wa Libuna.[#Yer. 52:1-3.]
19Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kama yote, Yoyakimu aliyoyafanya.[#2 Fal. 23:37.]
20Kwani ikawa kwa ajili ya makali ya Bwana yaliyouwakia mji wa Yerusalemu, hata nchi ya Yuda, akiwatupa, waondoke usoni pake. Kisha Sedekia akamkataa mfalme wa Babeli akiacha kumtii.[#2 Fal. 23:27.]