The chat will start when you send the first message.
1Lisikieni neno hili, ninyi ng'ombe wa Basani!
Ninyi mlioko milimani kwa Samaria
mkiwakorofisha wanyonge na kuwaponda maskini!
Ninyi mnaowaambia bwana zao: Haya! Leteni, tunywe!
2Bwana Mungu ameapa na kuutaja utukufu wake kwamba:
Mtaona, siku zikiwajia ninyi,
mtakapovutwa juu kwa kulabu,
hata masazo yenu yatavutwa juu kwa ndoana za kuvulia
samaki.
3Mtatoka penye nyufa za ukuta,
kila mwanamke mmoja ashike njia yake ya kwenda moja kwa
moja,
mje kujitupa huko Harmoni; ndivyo, asemavyo Bwana.
4Haya! Nendeni Beteli, mjikoseshe!
Nendeni Gilgali, mzidishe kujikosesha!
Katoeni asubuhi vipaji vyenu vya tambiko!
Hata kila siku ya tatu yatoeni mafungu yenu ya kumi!
5Chomeni mikate yenye chachu, iwe shukrani!
Tangazeni, visikilike, watu watoe vipaji viwapendezavyo!
Kwani ndivyo, mnavyovipenda, ninyi wana wa Isiraeli;
ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
6Nami niliwapa meno yakosayo kazi mijini mwenu mote
nao ukosefu wa mkate pote, mnapokaa, lakini hamkurudi
kwangu;
ndivyo, asemavyo Bwana.
7Tena mimi niliwanyima mvua,
miezi mitatu tu ilipokuwa imesalia mpaka mavunoni,
mji mmoja nikaunyeshea mvua, tena mwingine sikuunyeshea
mvua,
shamba moja likanyeshewa na mvua, jingine lisilopata mvua likakauka.
8Miji miwili mitatu ikatangatanga kuendea mji mmoja tu,
ndimo wapate kunywa maji, ijapo wasishibe, lakini
hamkurudi kwangu;
ndivyo, asemavyo Bwana.
9Nikawapiga ninyi, nikayaunguza mashamba na kuyakausha
kabisa,
tena mara nyingi nzige waliyala kwenu
mashamba na mizabibu na mikuyu na michekele yenu,
lakini hamkurudi kwangu;
ndivyo, asemavyo Bwana.
10Nilituma kwenu magonjwa mabaya, kama nilivyovifanya huko
Misri,
nikawaua vijana wenu kwa panga, nao farasi wenu
wakatekwa.
Nikaupandisha mnuko mbaya wa kambi zenu, uingie puani
mwenu,
lakini hamkurudi kwangu;
ndivyo, asemavyo Bwana.
11Niliwafudikiza wa kwenu, kama Mungu alivyofudikiza Sodomu
na Gomora,
mkawa kama kijinga kilichopona kwa kuokolewa,
kisiteketee chote motoni, lakini hamkurudi kwangu;
ndivyo, asemavyo Bwana.
12Kwa hiyo yako, nitakayokufanyizia Isiraeli;
jiweke tayari kukutana na Mungu wako, Isiraeli,
kwa ajili yao nitakayokufanyzia!
13Kwani utamwona atengenezaye milima, aumbaye upepo,
amwambiaye mtu ayawazayo moyoni mwake,
ni yeye ayageuzaye mapema kuwa giza
akipita na kukanyaga juu ya vilima vya nchi;
Bwana Mungu Mwenye vikosi ni Jina lake.