The chat will start when you send the first message.
1Mfalme Ahaswerosi akatoza kodi katika hiyo nchi, hata katika visiwa vya baharini.
2Matendo yote ya uwezo wake na ya nguvu zake na habari zote za macheo makuu, mfalme aliyompa Mordekai, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wao Wamedi na Wapersia?[#Est. 8:2,15.]
3Kwani Myuda Mordekai alikuwa wa pili kwake mfalme Ahaswerosi na mkuu kwa Wayuda, akapendwa na ndugu zake waliokuwa wengi, kwa kuwa aliwatakia mema walio ukoo wake, akasema nao wote walio wa kizazi chake maneno ya utengemano.