The chat will start when you send the first message.
1Nyote mwonao kiu, njoni kwenye maji!
Nanyi mkosao fedha, njoni kununua, mpate kula!
Nunueni pasipo fedha bure tu mvinyo na maziwa!
2Mbona mnatoa fedha pasipo kupata chakula?
Nayo mapato yaliyowachokesha
mbona mnayatoa pasipo kushiba?
Nisikilizeni, mpate kula mema,
roho zenu zipendezwe na manono!
3Yategeni masikio yenu! Njoni kwangu, mnisikie,
roho zenu zipate kupona!
Nami nitafanya nanyi agano la kale na kale
la kuwapa magawio ya Dawidi yanayotegemeka.
4Jueni! Nimemweka kunishuhudia kwa makabila ya watu,
akawa mkuu na mtawala makabila ya watu.
5Tazama! Utaita watu, usiowajua,
nao watu wasiokujua watakukimbilia,
kwa kuwa uko na Bwana Mungu wako,
kwa kuwa Mtakatifu wa Isiraeli amekupa utukufu.
6*Mtafuteni Bwana, akingali yuko, aoneke!
Mwiteni, akingali karibu!
7Asiyemcha Mungu na aiache njia yake,
kila mtu na auache upotovu wa mawazo yake!
Na arudi kwake Bwana Mungu wetu, amhurumie!
Kwani huzidisha kutuondolea mabaya.
8Kwani ndivyo, asemavyo Bwana:
Mawazo yangu siyo mawazo yenu,
wala njia zenu sizo njia zangu;
9kama mbingu zilivyo juu kabisa kuliko nchi,
ndivyo, njia zangu zilivyo juu kabisa kuliko zenu,
ndivyo, nayo mawazo yangu yalivyo makuu
kuliko mawazo yenu.
10Kwani kama mvua ya maji na ya mawe
inavyoshuka toka mbinguni,
isirudi huko, isipokwisha kuinywesha nchi
na kuizalisha na kuichipuza,
itoe mbegu za kupanda na vilaji vya kula:
11ndivyo, litakavyokuwa Neno langu
litokalo kinywani mwangu,
nalo halitarudi kwangu bure
lisipokwisha kufanya yanipendezayo,
lipate kuyatimiza,
ambayo nililituma kuyafanya.*
12Kwani mtatoka na kufurahi,
mtaongozwa, mwende na kutengemana.
Milima navyo vilima vitapaza sauti
za kushangilia mbele yenu,
hata miti yote ya porini itapiga makofi.
13Palipokuwa na mikunju tu, patakuwa na mivinje,
napo palipokuwa na viwawi tu, patakuwa na miti ya vihagilo,
nayo miti hiyo italitangaza Jina la Bwana,
iwe kielekezo chake cha kale na kale kisichong'oleka.