The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo Iyobu, yasikilize nitakayoyasema! Maneno yangu yote yategee masikio yako!
2Tazama! Nitakifumbua kinywa changu, ulimi wangu useme kinywani mwangu.
3Maneno yangu yananyoka kama moyo wangu; midomo yangu itayasema ninayoyajua, yaliyo ya kweli.
4Roho ya Mungu aliyeniumba na pumzi ya Mwenyezi zinanipa kuwapo.
5Kama utaweza na unijibu! Jiweke tayari kusimama usoni pangu!
6Tazama! Mimi na wewe kwake Mungu tu sawa, mimi nami nilifinyangwa kwa udongo.[#Iy. 10:9.]
7Tazama! Sikutishi, usinistukie, nayo nitakayokutwika yasikulemeze.
8Kweli ulisema masikioni pangu, nikaisikia sauti yao hayo maneno:
9Ninatakata, sikufanya kiovu, mimi ni safi, sikukora manza.[#Iy. 16:17; 27:6.]
10Tazama! Yako mambo, Mungu aliyonionea: ananiwazia kuwa miongoni mwao wachukivu wake.[#Iy. 13:24; 19:11.]
11Anaitia miguu yangu mikatale, anapaangalia pote, nipitapo.[#Iy. 13:27.]
12Tazama! Ninakujibu: kwa hiyo huongoki, kwani Mungu ni mkuu kuliko mtu.
13Mbona unamgombeza kwa kusema: Hayo yote hajibu neno liwalo lote?
14Lakini Mungu akisema mara moja au mara mbili, mtu haangalii; au sivyo?
15Watu wakiona ndoto kwa kulala usiku wenye usingizi mwingi, hapo, wanapokuwa wanalala vitandani pao,
16ndipo, anapoyazibua masikio ya watu, ayatie muhuri hayo, aliyowafunza na kuwaonya,[#Iy. 36:10; Sh. 16:7.]
17amkataze mtu kuyafanya tena, aliyoyafanya, ayakinge majivuno, yasimpate mtu;[#Sh. 119:67,71.]
18aizuie nayo roho yake, isitumbukie shimoni, nao mwili wake wenye uzima, usipite penye mishale iuayo.
19Kwa hiyo mtu anachapwa na kuumizwa kitandani pake, mifupa yake ikishindana na mateso pasipo kukoma.
20Huchafukwa na moyo anapokula, ijapo kiwe chakula hicho, anachokitamani rohoni.
21Nyama za mwili wake zinakauka, zisionekane, mifupa yake iliyokuwa haionekani ikatokea waziwazi.
22Roho yake ikafika karibu kuingia shimoni, nao moyo wake ukawafikia wauuao.
23Hapo malaika akamtokea, ampatanishe na Mungu, mmoja wao walioko kama elfu; akimwonyesha mtu njia ya kunyoka tena,[#Ebr. 1:14.]
24ndipo, atakapomhurumia na kumwambia: Mwokoe huyu, asishuke shimoni! Kwani makombozi yake nimeyapata.
25Ndipo, nyama za mwili wake zitakapochipuka kuliko zile za utoto, azirudie kuwa kama siku hizo za ujana wake.[#Sh. 103:5.]
26Atakapomwomba Mungu, atapendezwa naye, atamwonyesha uso wake, aushangilie; ndivyo, anavyompatia mtu kuwa mwongofu tena.
27Naye ataimba, watu wamsikie, akiungama kwamba: Nalikosa kwa kuyapotoa yanyokayo, lakini hakuna malipo, niliyotozwa!
28Akaikomboa roho yangu, isitumbukie shimoni, moyo wangu uufurahie huu mwanga![#Iy. 33:18.]
29Tazama! Hayo yote ndiyo, Mungu anayoyafanya mara mbili, hata mara tatu,
30airudishe roho ya mtu, isitumbukie shimoni, mwanga wenye uzima umwangazikie.[#Sh. 56:13; 103:4.]
31Tega masikio, Iyobu, unisikilize! Nyamaza tu, mimi niseme!
32Kama unaona la kusema, nijibu! Sema! Kwani nitapendezwa kukuona kuwa mwenye wongofu.
33Kama wewe huna la kusema, nisikilize! Nyamaza tu, nikufunze werevu ulio wa kweli!
Elihu akajibu tena akisema: