The chat will start when you send the first message.
1*Kwani mtaiona hiyo siku, ikija na kuwaka moto kama wa tanuru; ndipo, waliomsahau Mungu nao wote waliofanya maovu watakapokuwa makapi, siku hiyo ijayo itakapoyateketeza, isisaze wala mizizi wala matawi yao hao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
2Lakini ninyi mliogopao Jina langu jua la wongofu litawachea, nalo litakuwa linao uponya mabawani mwake; ndipo, mtakapochezacheza kama ndama watokao zizini.[#Luk. 1:78.]
3Nao wasiomcha Bwana mtawaponda na kuwakanyagakanyaga, kwani watageuka kuwa uvumbi chini ya nyayo za miguu yenu siku hiyo, nitakayoifanya mimi.[#Mal. 3:17.]
4Yakumbukeni Maonyo ya mtumishi wangu Mose, niliyomwagiza kule Horebu, awafundishe Waisiraeli wote maongozi na maagizo.
5Na mwone, nikimtuma mfumbuaji Elia kuja kwenu, siku kubwa ya Bwana iogopeshayo itakapokuwa haijatimia bado.[#Yoe. 3:4; Mat. 11:14; 17:11-13.]
6Yeye ndiye atakayeigeuza mioyo ya baba, warudi kwa watoto, nayo ya watoto, warudi kwa baba zao, nisije kuipiga nchi na kuiapiza.*[#Luk. 1:17.]