The chat will start when you send the first message.
1Nikaona nyama mkali, akitoka baharini mwenye pembe kumi na vichwa saba; juu hizo pembe zake zilikuwa na vilemba kumi vya kifalme, napo vichwani pake palikuwa na majina ya kumtukana Mungu.[#Ufu. 11:7; 17:3,9,12; Dan. 7:3,7.]
2Huyu nyama, niliyemwona, alifanana na chui, lakini miguu yake ilikuwa kama ya nyegere; nacho kinywa chake kilikuwa kama kinywa cha simba. Yule joka akampa uwezo wake na kiti chake cha kifalme na nguvu nyingi.[#Ufu. 12:3.]
3Miongoni mwa vichwa vyake nikaona kimoja kilichokuwa, kama kimepasuliwa kwa kuuawa, lakini donda lake la kuuawa lilikuwa limepona. Ulimwengu wote ukamtazama yule nyama na kumstuka,[#Ufu. 17:8.]
4kisha wakamwangukia yule joka, kwa sababu alimpa yule nyama nguvu zake, wakamwangukia naye yule nyama wakisema: Yuko nani anayefanana na nyama huyu? Tena yuko nani anayeweza kupiga vita naye?
5Kisha akapewa domo la kusema makuu ya kumtukana Mungu, akapewa nguvu ya kuyafanya hayo mambo yake miezi 42.[#Ufu. 11:2; 12:6,14; Dan. 7:8.]
6Ndipo, alipolifunua domo lake, amtukane Mungu, alitukane nalo Jina lake na tuo lake nao wakaao mbinguni.
7Tena akapewa kufanya vita nao watakatifu na kuwashinda, akapewa nguvu ya kushinda hata mashina na makabila na misemo na wamizimu wote.[#Ufu. 11:7; Dan. 7:21.]
8Kwa hiyo watamwangukia yeye wote wakaao nchini, ambao tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa, hawakuandikwa majina yao katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa.[#Ufu. 3:5; 12:12; 17:8.]
9Mtu akiwa na masikio na asikie![#Ufu. 14:12; Mat. 26:52.]
10Kama yuko mwenye kuteka, naye atatekwa; kama yuko mwenye kuua kwa upanga, naye sharti auawe kwa upanga. Hapo ndipo, watakatifu watakapovumilia kwa kumtegemea Mungu.
11Nikaona nyama mwingine, akitoka katika nchi; huyu alikuwa na pembe mbili kama mwana kondoo, akasema kama joka.[#Ufu. 16:13; Mat. 7:15.]
12Hata nguvu zote za yule nyama wa kwanza aliyemtangulia huzitumia, aishurutishe nchi nao wakaao nchini, wamwangukie yule nyama wa kwanza aliyepona donda lake la kuuawa.[#Ufu. 13:2,4,5,7.]
13Hufanya vielekezo vikubwa, hata kushusha moto toka mbinguni, uanguke nchini machoni pa watu.[#1 Fal. 18:24-39; Mat. 24:24; 2 Tes. 2:9-10.]
14Kwa hivyo vielekezo, alivyopewa kuvifanya mbele ya yule nyama, huwadanganya wakaao nchini akiwaambia wale wakaao nchini, wafanye kinyago cha mfano wa yule nyama aliyekuwa na kidonda cha upanga, akapata kupona.[#5 Mose 13:1-3.]
15Kisha akapewa kukitia pumzi kinyago cha yule nyama, hicho kinyago cha yule nyama kiseme; kwa hiyo nguvu yake wakauawa wote wasiokiangukia kinyago hicho cha yule nyama.
16Kwani anawashurutisha wote, wadogo na wakubwa, wenye mali na wakosao mali, waungwana na watumwa, wajitie chapa mikononi mwao mwa kuume au mapajini pao,[#Ufu. 19:20.]
17maana mtu asiweze kununua au kuuza kitu, asipokuwa na chapa cha jina la yule nyama au kiwango cha jina lake.
18Hapa ndipo panapotakwa werevu wa kweli; aliye mwenye akili na akifumbue kiwango cha yule nyama! Nacho kiwango chake ndicho mia sita na sitini na sita (666).[#Ufu. 15:2; 17:9.]