The chat will start when you send the first message.
1Nikaona kielekezo kingine mbinguni kilicho kikubwa cha kustaajabu, ni malaika saba walioyashika mapigo saba ya mwisho, kwani katika hayo ndimo, makali ya Mungu yalimotimia.[#Ufu. 11:18; 12:1,3; 16:1.]
2Nikaona yaliyokuwa kama bahari ya kioo iliyochanganyika na moto. Nikawaona wale walioshinda katika maumivu ya yule nyama na ya kinyago chake na ya kiwango cha jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya bahari ya kioo wakishika mazeze ya Mungu.[#Ufu. 4:6; 5:8; 13:15-18.]
3Wakaimba wimbo wa Mose aliyekuwa mtumwa wake Mungu na wimbo wa Mwana kondoo wakisema:
Kazi zako ni kuu na za kustaajabu, Bwana Mungu Mwenyezi!
Njia zako ni za wongofu na za kweli, mfalme wa wamizimu!
4Yuko asiyekuogopa wewe, Bwana?
Au yuko asiyelitukuza Jina lako?
Kwani wewe peke yako umetakata,
wamizimu wote watakuja na kukuangukia mbele yako,
kwa kuwa vimetokea waziwazi, unavyowapa watu wongofu.
5Kisha nikaona Jumba la Mungu, lile Hema la Ushahidi lililoko mbinguni, lilivyofunguliwa.[#Ufu. 11:19; Ebr. 9:24.]
6Humo Jumbani mwa Mungu wakatoka wale malaika saba; walioyashika yale mapigo saba; walikuwa wamevaa nguo nyeupe zimetukazo, napo vifuani walikuwa wamefunga mikanda ya dhahabu.[#Ufu. 1:13.]
7Ndipo, mmoja wao wale nyama wanne alipowapa hao malaika saba vyano saba vya dhahabu vilivyojaa makali yake Mungu aliye mwenye kuishi kale na kale pasipo mwisho.[#Ufu. 4:6-8; 14:10.]
8Kisha Jumba la Mungu likajaa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na kwenye uwezo wake. Hakuwako hata mmoja aliyeweza kuingia Jumbani mwa Mungu, mpaka yale mapigo saba ya wale malaika saba yatakapotimilika.[#2 Mose 30:34; 1 Fal. 8:10; Yes. 6:4; Ez. 44:4.]