The chat will start when you send the first message.
1Tena akafanya madhabahu ya shaba, mikono ishirini urefu wake, na mikono ishirini upana wake, na mikono kumi kwenda juu kwake.[#Kut 27:1; 1 Fal 9:25; 2 Fal 16:14; Eze 43:13]
2Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa mikono mitano; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.[#Kut 30:18; 1 Fal 7:23]
3Na chini yake palikuwa na mifano ya ng’ombe, walioizunguka pande zote, kwa mikono kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Ng’ombe walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.[#1 Fal 7:24; #4:3 Au, maboga (1 Wafalme 7:24).]
4Ikakaa juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
5Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.[#1 Fal 7:26]
6Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.[#1 Fal 7:38; Ebr 9:9]
7Akavifanya vinara vya taa kumi vya dhahabu, kadiri ya vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto.[#1 Fal 7:49; Kut 25:31]
8Akafanya na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia ya dhahabu.[#1 Fal 7:48]
9Tena akaufanya ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake.[#1 Fal 6:36]
10Nayo bahari akaiweka upande wa kuume kwa mashariki, kuelekea kusini.[#1 Fal 7:39]
11Na Huramu akayafanya masufuria, na majembe, na mabakuli.[#1 Fal 7:40]
Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;
12zile nguzo mbili, na vimbe, na taji mbili zilizokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo;[#1 Fal 7:41]
13na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo.[#Kut 28:33,34; 1 Fal 7:20; Wim 4:13; Yer 52:23]
14Akayafanya na matako, na mabirika akafanya juu ya matako;[#1 Fal 7:27,43]
15bahari moja, na ng’ombe kumi na wawili chini yake.
16Masufuria pia, na majembe, na nyuma, na vyombo vyake vyote, Huramu akamfanyia mfalme Sulemani kwa nyumba ya BWANA, vya shaba iliyokatuka.[#1 Fal 7:14,45; #4:16 Au, Huramu babaye.]
17Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda.[#1 Fal 7:46]
18Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani.[#1 Fal 7:47]
19Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;[#1 Fal 7:48-50; 2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 5:2,3; Kut 25:30; 1 Nya 28:16]
20na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika;[#Kut 27:20,21]
21na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora;[#Kut 25:31; 37:20; 1 Fal 6:18-35]
22na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.[#1 Fal 6:31]