The chat will start when you send the first message.
1Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari.[#Mwa 10:5; Zab 72:10; Isa 24:15]
2Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
3Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.[#Mwa 41:40; 2 Nya 28:7; Neh 2:10; Zab 122:8; Mit 12:20; Isa 26:12]