Yer 47

Hukumu juu ya Wafilisti

1Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. 2:4-7; Zek 9:5-7[#Isa 14:29-31; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef]

2BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe.[#Isa 8:7; Yer 1:14]

3Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;[#Nah 3:2]

4kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.[#Yer 25:22; Yoe 3:4; Amo 1:9,10; 9:7; Mwa 10:14]

5Upaa umeupata Gaza;[#Sef 2:4]

Ashkeloni umenyamazishwa

Mabaki ya bonde lao;

Hata lini utajikata-kata?

6Ee upanga wa BWANA,[#Eze 21:3]

Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?

Ujitie katika ala yako;

Pumzika, utulie.

7Utawezaje kutulia,[#1 Sam 3:12; Mik 6:9]

Ikiwa BWANA amekupa agizo?

Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,

Ndipo alipoyaamuru hayo.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania