Ufunuo 16

1NIKASIKIA sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vichupa vya ghadhabu ya Mungu juu ya inchi.

2Akaenda wa kwanza, akakimimina kichupa chake juu ya inchi, pakawa jipu baya, ovu, juu ya wale watu wenye alama ya nyama, na wale wenye kuisujudu sanamu yake.

3Malaika wa pili akakimimina kichupa chake juu ya bahari, pakawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho va uhayi vikafa katika bahari.

4Malaika wa tatu akakimimina kichupa chake juu mito, na chemchemi za maji, zikawa damu.

5Nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, ee Bwana, ulioko, uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivu;

6kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii, nawe umewapa damu, wainywe; nao wamestahili.

7Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.

8Malaika wa nne akakimimina kichupa chake juu ya jua; likapewa kuwaunguza wana Adamu kwa moto.

9Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu.

10Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao,

11wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao, wala hawakuyatubia matendo yao.

12Malaika wa sita akakimimina kichupa chake juu ya mto ule mkubwa Eufrate, maji yake yakakauka illi njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

13Nikaona roho tatu za uchafu kama vyura zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule nyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo.

14Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi.

15Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.

16Akawakusanya hatta maliali paitwapo kwa Kiebrania, Armageddon.

17Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.

18Pakawa sauti na radi na umeme, na palikuwa tetemeko la inchi, kubwa, ambalo tangu wana Adamu kuwako juu ya inchi halikuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.

19Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ilianguka: na Babeli ule mkuu nkakumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.

20Killa kisiwa kikakimbia, na milima haikuonekana tena.

21Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kuloka mbinguni juu ya wana Adamu. Wana Adamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe. Maana pigo lake kubwa mno.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania