The chat will start when you send the first message.
1Katika taabu yangu nilimwita Mwenyezi-Mungu,
naye akanijibu.
2Uniokoe ee Mwenyezi-Mungu,
na watu wadanganyifu na waongo.
3Enyi watu wadanganyifu, mtapewa kitu gani?
Mtaadhibiwa namna gani?
4Kwa mishale mikali ya askari,
kwa makaa ya moto mkali!
5Ole wangu kwamba naishi kama mgeni huko Mesheki;
naishi kama mgeni katika mahema ya Kedari.
6Nimeishi muda mrefu mno
kati ya watu wanaochukia amani!
7Wakati ninaposema nataka amani,
wao wanataka tu vita.