2 Wamakabayo 11

2 Wamakabayo 11

Yuda Makabayo amshinda Lisia

(1Mak 4:26-35)

1Mara baada ya hayo, si muda mrefu baada ya Timotheo kushindwa, Lisia, mlinzi na ndugu ya mfalme na mkuu wa serikali, alipata habari hizo. Alikasirika sana,

2akaongoza askari wa miguu 80,000 na wapandafarasi wake wote dhidi ya Wayahudi. Alikuwa na shabaha ya kuufanya mji wa Yerusalemu makao ya Wagiriki,

3na kulitoza kodi hekalu, kama mahali pengine pote pa ibada ya watu wa mataifa mengine. Na ukuhani mkuu ungenadiwa kila mwaka.

4Lisia hakujali chochote juu ya uwezo wa Mungu, bali alijivunia makumi elfu ya askari wake wa miguu, maelfu ya wapandafarasi wake, na tembo wake themanini.

5Hivi akaivamia Yudea na kuishambulia ngome ya Beth-zuri, yapata kilomita thelathini kusini ya Yerusalemu.

6Yuda Makabayo na watu wake waliposikia kwamba Lisia alikuwa anazizingira ngome zao, wakalia na kuomboleza pamoja na watu wote, wakimsihi Bwana amtume malaika mwema awaokoe.

7Yuda Makabayo alikuwa wa kwanza kuchukua silaha, akawahimiza wengine wajiunge naye katika kutoa mhanga maisha yao ili kuwasaidia Wayahudi wenzao. Hivi, wakatoka pamoja naye kwa ari na motomoto kabisa.

8Lakini, kabla hawajaenda mbali na Yerusalemu, kwa ghafla wakagundua kwamba walikuwa wanaongozwa na mpandafarasi mwenye mavazi meupe, amechukua silaha za dhahabu.

9Mara, wote kwa pamoja, wakamshukuru Mungu kwa huruma yake; alikuwa amewatia ujasiri wa kutosha kwa kushambulia si binadamu tu, bali pia wanyama wakali na hata kuta za chuma.

10Basi, wakaenda mbele wamejipanga kivita, wakiwa pamoja na yule msaidizi kutoka mbinguni, maana Bwana alikuwa amewaonea huruma.

11Kama simba, waliwarukia maadui zao na kuwaangusha askari wa miguu 11,000, na wapandafarasi 1,600, na kuwafanya wengine wakimbie.

12Wengi wa hao waliokimbia walikuwa wamejeruhiwa na kupoteza silaha zao. Hata Lisia mwenyewe alikimbia kwa aibu.

Lisia apatana na Wayahudi

(1Mak 6:56-61)

13Lisia, kwa vile hakuwa mjinga, alitafakari juu ya kushindwa kwake vitani, akatambua kwamba Wayahudi walikuwa hawashindiki kwa sababu Mungu Mwenye Nguvu alikuwa amewapigania. Kwa hiyo akapeleka ujumbe,

14akawashawishi wakubali kupatana kwa masharti ya haki, na akaahidi kumshawishi mfalme awe rafiki wao.

15Kwa manufaa ya watu wake, Yuda Makabayo akayakubali mapendekezo yote ya Lisia, kwa vile mfalme alikuwa ameyapokea na kuyakubalia maombi yote ambayo Yuda alikuwa amempa Lisia kwa maandishi.

Barua ya Lisia kwa Wayahudi

16Ifuatayo ni barua ambayo Lisia aliwaandikia Wayahudi:

Barua ya mfalme kwa Lisia

22Na barua ya mfalme ilikuwa kama ifuatavyo:

27Ifuatayo ni barua ya mfalme kwa taifa la Wayahudi:

Barua ya Waroma kwa Wayahudi

34Waroma nao waliwaandikia Wayahudi barua ifuatayo:

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania