Zaburi 126

Zaburi 126

Kuomba nguvu mpya

1Mwenyezi-Mungu alipoturekebisha na kuturudisha Siyoni,[#126:1 Maneno haya aghalabu yahusu Waisraeli waliporudi kutoka uhamishoni kule Babuloni.]

tulikuwa kama watu wanaoota ndoto!

2Hapo tuliangua kicheko;

tulishangilia kwa furaha.

Nao watu wa mataifa mengine walisema:

“Mwenyezi-Mungu amewatendea mambo makubwa!”

3Kweli Mwenyezi-Mungu alitutendea mambo makubwa,

tulifurahi kwelikweli!

4Ee Mwenyezi-Mungu, urekebishe tena hali yetu,

kama mvua inavyotiririsha maji katika mabonde makavu.

5Wanaopanda kwa machozi,

watavuna kwa shangwe.

6Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia,

watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania