The chat will start when you send the first message.
1Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote,
enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.
2Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu,
na kumtukuza Mwenyezi-Mungu!
3Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni;[#134:3 Maneno haya huenda yalitamkwa na kuhani kuwatakia baraka mahujaji waliofika Yerusalemu kwa sikukuu fulani. Taz pia 104.]
yeye aliyeumba mbingu na dunia.