Zaburi 150

Zaburi 150

Zaburi ya kumsifu Mungu

1Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Msifuni Mungu katika patakatifu pake;

msifuni katika mbingu zake kuu.

2Msifuni kwa sababu ya matendo yake makuu;

msifuni kwa ajili ya utukufu wake mkuu.

3Msifuni kwa mlio wa tarumbeta;

msifuni kwa zeze na kinubi!

4Msifuni kwa ngoma na kucheza;

msifuni kwa filimbi na banjo!

5Msifuni kwa kupiga matoazi.

msifuni kwa matoazi ya sauti kubwa.

6Kila kiumbe hai kimsifu Mwenyezi-Mungu!

Msifuni Mwenyezi-Mungu!

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania