Zaburi 93

Zaburi 93

Mungu mfalme

1Mwenyezi-Mungu anatawala;

amejivika fahari kuu!

Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu!

Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.

2Kiti chako cha enzi ni imara tangu kale;

wewe umekuwapo kabla ya nyakati zote.

3Vilindi vimetoa sauti, ee Mwenyezi-Mungu;

naam, vimepaza sauti yake,

vilindi vyapaza tena mvumo wake.

4Mwenyezi-Mungu ana enzi kuu juu mbinguni,[#93:3-4 Hapa, uwezo wa Mwenyezi-Mungu juu ya nguvu za fujo na maangamizi unatukuzwa. Vilindi (vya maji) na mawimbi ya maji (mafuriko) vyote vyahusu fujo ya kale na kale ambayo Mwenyezi-Mungu aliishinda wakati wa kuumba ulimwengu (taz pia 74:13-14; 89:9-10).]

ana nguvu kuliko mlio wa bahari,

ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.

5Ee Mwenyezi-Mungu, maagizo yako ni thabiti;

nyumba yako ni takatifu milele na milele.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania