1 Nyakati 6

1 Nyakati 6

Wana wa Lawi

1Wana wa Lawi walikuwa:

2Wana wa Kohathi walikuwa:

3Amramu alikuwa na wana:

Haruni alikuwa na wana:

16Wana wa Lawi walikuwa:

17Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:

18Wana wa Kohathi walikuwa:

19Wana wa Merari walikuwa:

20Wazao wa Gershoni:

22Wazao wa Kohathi:

25Wazao wa Elkana walikuwa:

28Wana wa Samweli walikuwa:

29Wafuatao ndio wazao wa Merari:

31Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana , baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, hadi hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

Kutoka koo za Wakohathi walikuwa:

39na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:

44Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:

48Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.

49Lakini Haruni na uzao wake ndio walikuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Musa mtumishi wa Mungu.

50Hawa walikuwa wazao wa Haruni:

55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na maeneo ya malisho yanayouzunguka.

56Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57Kwa hiyo wazao wa Haruni walipewa miji ifuatayo: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,

58Hileni, Debiri,

59Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

60Kutoka kabila la Benyamini, walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

61Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62Wazao wa Gershoni, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali, na kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63Wazao wa Merari, kufuatana na koo zao walipewa miji kumi na mbili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

65Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

67Katika nchi ya vilima ya Efraimu, walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,

68Yokmeamu, Beth-Horoni,

69Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

70Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

Katika nusu ya kabila la Manase, walipokea Golani katika Bashani, na pia Ashtarothi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

72Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi,

73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

74Kutoka kabila la Asheri, walipokea Mashali, Abdoni,

75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

76Kutoka kabila la Naftali, walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

kutoka kabila la Zabuloni, walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

78Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa,

79Kedemothi na Mefaathi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

80Na kutoka kabila la Gadi, walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu,

81Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.