Ezekieli 48

Ezekieli 48

Mgawanyo wa nchi

“Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja; mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi; Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

2Asheri atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi.

3Naftali atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi.

4Manase atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi.

5Efraimu atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi.

6Reubeni atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi.

7Yuda atakuwa na sehemu moja; itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.

8“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa elfu ishirini na tano, nao urefu wake kuanzia mashariki hadi magharibi utakuwa sawa na sehemu moja ya kabila; mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.[#48:8 Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25.]

9“Hiyo sehemu maalum mtakayotoa kwa Bwana itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi.[#48:9 Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5.]

10Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kaskazini, upana wa dhiraa elfu kumi upande wa magharibi, dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Bwana .

11Hii itakuwa kwa ajili ya makuhani waliowekwa wakfu, Wasadoki, waliokuwa waaminifu katika kunitumikia, nao hawakupotoka kama Walawi walivyofanya wakati Waisraeli walipopotoka.

12Itakuwa toleo maalum kwao kutoka sehemu takatifu ya nchi, yaani sehemu takatifu sana, inayopakana na nchi ya Walawi.

13“Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi.

14Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana .

15“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa elfu tano, na urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na maeneo ya malisho. Mji utakuwa katikati yake[#48:15 Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25.]

16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa elfu nne na mia tano, upande wa kusini dhiraa elfu nne na mia tano, upande wa mashariki dhiraa elfu nne na mia tano, na upande wa magharibi dhiraa elfu nne na mia tano.[#48:16 Dhiraa 4,500 ni sawa na kilomita 2.025.]

17Eneo la malisho kwa ajili ya mji litakuwa na eneo la dhiraa mia mbili na hamsini upande wa kaskazini, dhiraa mia mbili na hamsini upande wa kusini, dhiraa mia mbili na hamsini upande wa mashariki, na dhiraa mia mbili na hamsini upande wa magharibi.[#48:17 Dhiraa 250 ni sawa na sentimita 112.5.]

18Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa elfu kumi upande wa mashariki, na dhiraa elfu kumi upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula.

19Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli.

20Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani dhiraa elfu ishirini na tano kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.

21“Eneo linalobaki pande mbili za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu anayetawala. Eneo hili litaenea upande wa mashariki, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki, na kuelekea upande wa magharibi, kuanzia kwenye dhiraa elfu ishirini na tano hadi mpaka wa magharibi. Maeneo haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake.

22Kwa hiyo milki ya Walawi na milki ya mji vitakuwa katikati ya eneo lile ambalo ni mali ya mkuu anayetawala. Eneo la mkuu anayetawala litakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini.

“Benyamini atakuwa na sehemu moja; itakayoanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

24Simeoni atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Benyamini kuanzia mashariki hadi magharibi.

25Isakari atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Simeoni kuanzia mashariki hadi magharibi.

26Zabuloni atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Isakari kuanzia mashariki hadi magharibi.

27Gadi atakuwa na sehemu moja; itakayopakana na nchi ya Zabuloni kuanzia mashariki hadi magharibi.

28Mpaka wa kusini wa Gadi utapita kusini kuanzia Tamari hadi maji ya Meriba-Kadeshi, kisha kupitia upande wa Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu.[#48:28 yaani Bahari ya Mediterania]

Malango ya mji mpya

“Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu,

31malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.

32Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Yusufu, lango la Benyamini na lango la Dani.

33Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.

34Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.

“Nalo jina la mji huo kuanzia wakati huo na kuendelea litakuwa: ‘Bwana yupo hapa.’ ”

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.