Yona 3

Yona 3

Yona aenda Ninawi

1Ndipo neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili:

2“Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”

3Yona akalitii neno la Bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka.

4Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”

5Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa gunia.

6Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha utawala, akavua majoho yake ya mfalme, akajifunika gunia na kuketi mavumbini.

7Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote:

10Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.