Filemoni 1

Filemoni 1

Salamu

Shukrani na maombi

4Siku zote ninamshukuru Mungu wangu ninapokukumbuka katika maombi yangu,

5kwa sababu ninasikia kuhusu imani yako katika Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu wote.

6Naomba utiwe nguvu katika kushiriki imani yako na wengine, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu wa kila kitu chema tunachoshiriki kwa ajili ya Kristo.

7Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.

Paulo anamtetea Onesimo

8Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningekuwa na ujasiri wa kukuagiza yale yakupasayo kutenda,

9lakini ninakuomba kwa upendo. Mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Kristo Yesu,

10nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.[#1:10 maana yake Wa manufaa]

11Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.

12Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa.

13Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.

14Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari.

15Huenda sababu ya Onesimo kutengwa nawe kwa muda ni ili uwe naye daima,

16si kama mtumwa sasa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana.

17Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika nawe, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe.

18Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi.

19Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa hilo deni. Kumbuka kwamba nakudai hata nafsi yako.

20Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana, yaani uniburudishe moyo wangu katika Kristo.

21Huku nikiwa na hakika ya kutii kwako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.

22Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu.

Salamu za mwisho

23Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu, anakusalimu.

24Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu.

25Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.