Ayubu 25

Ayubu 25

Bildadi anena: Mtu awezaje kuwa mwenye haki mbele za Mungu

1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,

2Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;[#25:2 Katika Kiebrania ni naye.]

Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.

3Je! Majeshi yake yahesabika?[#Mwa 1:3-5,14-16; Zab 19:4-6; 139:8,11; Mt 5:45; Yak 1:17]

Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?

4Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?[#Ayu 4:17; 9:2; Zab 130:3; 143:2; Rum 3:19,20]

Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?

5Tazama, hata mwezi hauangazi,

Wala nyota si safi machoni pake;

6Sembuse mtu, aliye mdudu![#Zab 22:6]

Na mwanadamu, ambaye ni buu!

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania