The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,[#2 Fal 25:8-10; 2 Nya 36:17-19; Yer 26:18; 52:12-14]
Wamelinajisi hekalu lako takatifu.
Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.
2Wameziacha maiti za watumishi wako[#Yer 7:33]
Ziwe chakula cha ndege wa angani.
Na miili ya watauwa wako
Iwe chakula cha wanyama wa nchi.
3Wamemwaga damu yao kama maji[#Ufu 11:9]
Pande zote za Yerusalemu,
Wala hapakuwa na mtu wa kuwazika.
4Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
5Ee BWANA, hadi lini? Utaona hasira milele?[#Kum 29:20; Eze 36:5]
Wivu wako utawaka kama moto?
6Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,[#Isa 45:4; Zab 53:4]
Na falme za hao wasioliitia jina lako.
7Kwa maana wamemla Yakobo,
Na makao yake wameyaharibu.
8Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,[#Isa 43:25]
Rehema zako zije kutulaki haraka,
Kwa maana tumeteseka sana.
9Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,[#Yos 10:6; Yer 14:7]
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utusamehe dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako.
10Kwa nini mataifa yaseme,
Yuko wapi Mungu wao?
Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika
Kijulikane kati ya mataifa machoni petu.
11Kuugua kwake aliyefungwa[#Hes 14:17]
Na kuingie mbele zako.
Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako
Uwahifadhi waliohukumiwa kufa.
12Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao
Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.
13Na sisi tulio watu wako,[#Isa 43:21]
Na kondoo za malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi hadi kizazi.