Zaburi 82

Zaburi 82

Ombi la kupata haki

1Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;[#Mhu 5:8; Kut 21:6]

Katikati ya miungu anahukumu.

2Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma,

Na kuzikubali nyuso za wabaya?

3Mfanyieni hukumu maskini na yatima;[#Kum 1:17; Zab 58:1,2]

Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;

4Mwokoeni maskini na mhitaji;

Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

5Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;[#Zab 11:3]

Misingi yote ya nchi imetikisika.

6Mimi nimesema, Ndinyi miungu,[#Ayu 21:32; Eze 31:14; Yn 10:34]

Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.

7Lakini mtakufa kama wanadamu,

Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

8Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,[#Zab 2:8; Ufu 11:15]

Maana mataifa yote ni yako.

The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013. 
Published by: Bible Society of Tanzania