The chat will start when you send the first message.
1Wote walio katika mafungo ya utumwa sharti wawape mabwana zao heshima zote, Jina la Mungu nao ufundisho wetu usifyozwe![#Ef. 6:5; Tit. 2:9-10.]
2Lakini walio wa mabwana wenye kumtegemea Mungu wasiwabeze, kwa kwamba ni ndugu, ila wawatumikie kupita wengine, kwa sababu nao wamemtegemea Mungu! Inafaa, wapendwe, maana nao hutaka kuwafanyizia kazi njema.[#1 Tes. 1:4; File. 16.]
3Mtu akifundisha mengine, asiposhikamana na maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo yatupayo uzima wala na ufundisho upasao wenye kumcha Mungu,[#Gal. 1:6-9; 2 Tim. 1:13.]
4basi, mtu huyo ametutumka, hana, akijuacho, kilema chake ni mashindano na mabishano ya kujisemea tu. Hayo ndiyo yanayoleta wivu na ugomvi na matusi na masingizio mabaya
5na machukivu yasiyokoma. Hao huwa kama wenye wazimu waepukao kabisa kwenye kweli, ndio wanaodhani kwamba: Kumcha Mungu ni chumo. Walio hivyo jitenge nao!
6*Kweli kumcha Mungu ni chumo kubwa, kukiwa pamoja na kutoshewa nayo, tuliyo nayo.[#1 Tim. 4:8; Mat. 6:25-34; Fil. 4:11-12; Ebr. 13:5.]
7Kwani hakuna, tulichokileta humu ulimwenguni, wala hakuna, tuwezacho kutoka nacho tena.[#Iy. 1:21; Mbiu. 5:15.]
8Lakini tukiwa na vyakula na vya kuvaa tuseme: Vinatutoshea![#Fano. 30:8.]
9Lakini wanaotaka kupata mali nyingi huanguka penye majaribu na matanzi na tamaa nyingi zisizo na maana, ziponzazo watu na kuwatumbukiza maangamizoni, wanapopata kuoza tu.[#Fano. 23:4; 28:22.]
10Kwani choyo ni shina la maovu yote. Wengine walikifuata, wakapotelewa, wasiweze kumtegemea Mungu tena, wakajipatia maumivu mengi.[#Ef. 5:5.]
11Lakini wewe uliye mtu wa Mungu hayo yakimbie! Ukimbilie wongofu na kumcha Mungu na kumtegemea na kupendana na kuvumilia na kujinyenyekeza![#Fil. 3:12-14; 2 Tim. 2:22; Ebr. 3:1; 10:23.]
12Vipige vile vita vizuri vya kumtegemea Mungu! Ishike njia ya uzima wa kale na kale, ulioitiwa, ukaungama ungamo zuri mbele ya mashahidi wengi.*[#1 Kor. 9:25-26.]
13Nakuagiza mbele yake Mungu anayevipa vyote uzima na mbele ya Kristo Yesu aliyelishuhudia ungamo lake zuri mbele ya Pontio Pilato,[#Yoh. 18:36-37; 19:11.]
14uyalinde uliyoagizwa, yasiwe na doadoa wala kilema, mpaka bwana wetu Yesu Kristo atakapotokea;
15naye atakayemtokeza kwetu, siku zake zitakapotimia, ni yule anayeshangiliwa kuwa Mwenyezi peke yake, yule mwenye kutawala wafalme na mabwana.[#1 Tim. 1:11; 5 Mose 10:17; Ufu. 17:14.]
16Ni yeye peke yake asiyekufa, hukaa mwangani, msimofikiwa na mtu; hakuna mtu aliyemwona, wala hakuna awezaye kumtazama. Yeye aheshimiwe, kwa sababu nguvu ni zake kale na kale! Amin.[#2 Mose 33:20.]
17Walio wenye mali nyingi humu ulimwenguni waagize, wasijikweze, wala wasizitumainie mali, maana hutoweka upesi; ila sharti wamtumainie Mungu anayetupatia yote na kuyafurikisha, tushibe vema.[#Sh. 62:11; Luk. 12:15-21.]
18Waagize, wafanye mwenendo mwema wakifuliza kufanya kazi nzuri, wakigawia wengine mema yao kwa kuwa bia moja nao.
19Hivyo ndivyo, watakavyojiwekea malimbiko yatakayokuwa msingi mzuri, siku zitakapotimia za kuupata uzima ulio wa kweli.[#Mat. 6:20.]
20Timoteo, yalinde, uliyopewa ya kuyaweka! Yakatae yale mapuzi yaliyo ya bure tu nayo yale mabishano ya utambuzi ulio wa uwongo tu![#1 Tim. 4:7; 2 Tim. 1:14.]
21Maana wengine walioufuata wamepotelewa na njia ya kumtegemea Mungu. Upole uwakalie ninyi! Amin.[#1 Tim. 1:6; 2 Tim. 2:18.]