The chat will start when you send the first message.
1Yoabu alipopashwa habari kwamba: Tazama, mfalme analia na kumwombolezea Abisalomu,
2ndipo, wokovu wa siku hiyo ulipowageukia watu wote kuwa uchungu, kwani watu walisikia siku hiyo kwamba: Mfalme anamsikitikia mwanawe.
3Kwa hiyo wakaingia mjini siku hiyo na kujifichaficha kama wezi, wakawa kama watu wanaotoka vitani na kujifichaficha kama wezi, kwa kuwa wametoroka vitani.
4Mfalme akaufunika uso wake, naye mfalme akalia na kupaza sauti sana kwa kwamba: Mwanangu Abisalomu! Abisalomu mwanangu! Mwanangu!
5Ndipo, Yoabu alipoingia nyumbani mwa mfalme, akasema: Leo umezitia soni nyuso za watumishi wako wote, nao wameiponya leo roho yako nazo roho zao wanao wa kiume na wa kike nazo roho zao wake zako na masuria zako.
6Unawapenda wakuchukiao, ukawachukia wakupendao, kwani leo umevitokeza, ya kuwa wakuu na watumishi si kitu kwako, kwani leo nimevitambua hivi: kama Abisalomu angalikuwa mzima, kama sisi sote tungaliuawa, basi, hili jambo lingenyoka machoni pako.
7Lakini sasa inuka, utoke, useme na watumishi wako na kuituliza mioyo yao! Kwani ninaapa na kumtaja Bwana kwamba: Usipowatokea, hakuna mtu atakayelala kwako usiku huu, nayo mabaya yatakayokupata kwa ajili hii yatakuwa mabaya zaidi kuliko yote yaliyokupata tangu utoto wako mpaka sasa.
8Ndipo, mfalme alipoondoka, akaja kukaa langoni; nao watu walipowatangazia watu wote kwamba: Tazameni, mfalme amekaa langoni, watu wote wakaja kumtokea mfalme.
Lakini Waisiraeli walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake,
9Watu wote wakarudiana katika mashina yote ya Waisiraeli kwamba: Mfalme ametuponya mikononi mwa adui zetu, naye ndiye aliyetuponya mikononi mwa Wafilisti, naye hakuwa na budi kumkimbia Abisalomu na kutoka katika nchi hii.
10Naye Abisalomu, tuliyempaka mafuta, awe mfalme wetu, amekufa vitani; sasa mwakawiliaje tena kumrudisha mfalme?
11Kisha mfalme akatuma kwa watambikaji Sadoki na Abiatari kwamba: Waambieni wazee wa Waisiraeli kwamba: Mbona mwataka kuwa wa mwisho wa kumrudisha mfalme nyumbani mwake? Kwa maana lile shauri la Waisiraeli lilikuwa limefika nyumbani kwa mfalme.
12Ninyi m ndugu zangu, mifupa yetu ni ya mmoja, nazo nyama za miili yetu ni za mmoja; mbona mnataka kuwa wa mwisho wa kumrudisha mfalme?
13Naye Amasa mwambieni: Kumbe wewe na mimi mifupa yetu siyo ya mmoja, nazo nyama za miili yetu sizo za mmoja? Mungu na anifanyizie hivi na hivi, wewe usipopata kwangu kuwa mkuu wa vikosi siku zote mahali pake Yoabu![#2 Sam. 17:25; 1 Mambo 2:16-17.]
14Ndivyo, alivyojipatia tena mioyo ya Wayuda wote kuwa ya mtu mmoja tu, nao wakatuma kwa mfalme kumwambia: Rudi wewe pamoja na watumishi wako wote!
15Ndipo, mfalme aliporudi; alipofika Yordani, Wayuda walikuwa wamefika Gilgali kumwendea mfalme njiani, wamvushe mfalme Yordani.
16Naye Mbenyamini Simei, mwana wa Gera, aliyekaa Bahurimu, akaja upesi, akashuka pamoja na watu wa Yuda kumwendea mfalme Dawidi njiani.[#1 Fal. 2:8.]
17Pamoja naye wakaja watu elfu toka nchi ya Benyamini, hata Siba, mtumishi wa nyumbani mwa Sauli, akaja na wanawe 15 na watumishi wake 20. Wao walikuwa wamevuka Yordani, mfalme alipokuwa hajaja bado.[#2 Sam. 9:2,10; 16:1-4.]
18Mtumbwi wa kuwavusha walio wa nyumbani mwa mfalme ulipofika ng'ambo ya huko, mfalme aone, wanavyomfanyizia kazi nzuri, ndipo, Simei, mwana wa Gera, alipojiangusha chini machoni pa mfalme, alipotaka kuuvuka Yordani,
19akamwambia mfalme: Bwana wangu asiniwazie kuwa mwenye uovu, wala asiyakumbuke yale mapotovu, mtumwa wako aliyoyafanya siku ile, bwana wangu mfalme alipotoka Yerusalemu, bwana wangu mfalme asiyaweke moyoni![#2 Sam. 16:5.]
20Kwani mtumwa wako anajua, ya kuwa mimi nimekosa; kwa hiyo unaniona leo, ya kuwa mimi ni wa kwanza wa mlango wote wa Yosefu, aliyeshuka kumwendea bwana wangu mfalme njiani.
21Ndipo, Abisai, mwana wa Seruya, alipojibu na kusema: Je? Simei asiuawe kwa ajili ya hayo tu? Kwani alimtukana aliyepakwa mafuta na Bwana.
22Lakini Dawidi akasema: Tuna bia gani mimi nanyi wana wa Seruya, mkitaka kuniwia leo Satani? Ingekuwaje, mtu akiuawa leo kwa Waisiraeli? Kwani si leo, nilipopata kujua, ya kuwa mimi ni mfalme wa Waisiraeli?[#2 Sam. 16:10.]
23Kisha mfalme akamwambia Simei na kumwapia: Hutauwa kabisa!
24Naye Mefiboseti, mwana wa Sauli, akashuka kumwendea mfalme njiani. Naye alikuwa hakuiogesha miguu yake, wala hakuzikata ndevu zake za midomoni, wala hakuzifua nguo zake tangu siku ile, mfalme alipokwenda, hata siku hiyo, aliporudi na kutengemana.[#2 Sam. 9:6.]
25Ikawa, alipotoka Yerusalemu kumwendea mfalme njiani, mfalme akamwuliza: Sababu gani hukuenda pamoja na mimi, Mefiboseti?
26Akasema: Bwana wangu mfalme, mtumishi wangu alinidanganya, kwani mtumishi wako alisema: Nitajitandikia punda, nimpande, nipate kwenda pamoja na mfalme, kwani mtumishi wako ni kiwete.
27Lakini yule amemsingizia mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme, lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, na ufanye yaliyo mema machoni pako![#2 Sam. 17:17; 16:3.]
28Kwani wao wote wa mlango wa baba yangu walikuwa watu wa kufa tu mbele ya bwana wangu mfalme, lakini wewe walimweka mtumishi wako kwao wanaokula mezani pako; liko jambo gani tena linipasalo, nimlilie tena mfalme kwa ajili yake?[#2 Sam. 9:11.]
29Mfalme akamwambia: Unayasemaje haya maneno yako tena? Basi, mimi ninatoa amri hii: Wewe na Siba mgawane mashamba![#2 Sam. 9:9-10; 16:4.]
30Ndipo, Mefiboseti alipomwambia mfalme: Na ayachukue yote yeye! Kwa kuwa bwana wangu mfalme amefika nyumbani kwake na kutengemana.
31Naye Barzilai wa Gileadi alikuwa ameshuka toka Roglimu, akapita naye mfalme kufika Yordani, apate kumvusha huko Yordani.[#1 Fal. 2:7.]
32Naye Barzilai alikuwa mzee mwenye miaka 80, naye ndiye aliyemtunza mfalme, alipokaa Mahanaimu, kwani alikuwa mtu mkuu sana.[#2 Sam. 17:27.]
33Mfalme akamwambia Barzilai: Wewe fuatana na mimi, nami nikutunze kwangu Yerusalemu!
34Lakini Barzilai akamwambia mfalme: Siku za miaka yangu ya kuwapo ni ngapi, nipande kwenda Yerusalemu pamoja na mfalme?
35Mimi ni mwenye miaka 80 leo, nitawezaje kupambanua yaliyo mema nayo yaliyo mabaya? Au mtumishi wako atawezaje kuuona utamu wa vilaji, ninavyovila, nao wa vinywaji, ninavyovinywa? Au nitawezaje kuzisikiliza sauti zao waimbaji wa kiume na wa kike? Kwa hiyo mtumishi wako atatakaje kukulemea tena, bwana wangu mfalme?
36Kidogo tu mtumishi wako atamsindikiza mfalme, akiisha kuuvuka Yordani. Sababu gani mfalme anataka kunirudishia tendo hili kwa njia ile?
37Mwache mtumishi wako, arudi, nipate kujifia mjini kwangu kwenye kaburi la baba yangu na la mama yangu. Lakini tazama, huyu ni mtumishi wako Kimuhamu; yeye atakwenda huko pamoja na bwana wangu mfalme, umfanyizie yaliyo mema machoni pako.
38Mfalme akajibu: Basi, Kimuhamu atakwenda huko pamoja na mimi, nami nitamfanyizia yaliyo mema machoni pangu, nayo yote, utakayonitakia, nitakufanyizia.
39Watu wote walipokwisha kuuvuka Yordani, mfalme naye akavuka; kisha mfalme akamnonea Barzilai, naye akambariki, kisha akarudi mahali pake.
40Mfalme alipoendelea kwenda Gilgali, Kimuhamu akaenda naye. Watu wote wa Yuda walikuwa wamevuka pamoja na mfalme, hata nusu ya watu wa Waisiraeli.
41Mara watu wote wa Waisiraeli wakaja kwa mfalme, wakamwambia mfalme: Mbona ndugu zetu Wayuda wamekuiba, wakimvusha mfalme nao wa mlango wako kule Yordani nao watu wote wa Dawidi waliokuwa naye.
42Ndipo, watu wote wa Yuda walipowajibu Waisiraeli: Maana mfalme ni karibu kwetu; kwa sababu gani mnalichafukia jambo hili? Je? Tumekula mali za mfalme? Au ametupa tunzo lo lote?[#2 Sam. 19:11-12.]
43Ndipo, Waisiraeli walipowajibu Wayuda kwamba: Mafungu yetu sisi yaliyoko kwa mfalme ni kumi, kwa hiyo naye Dawidi ni wetu kuliko wenu. Mbona mmetubeua? Je? Shauri hilo la kumrudisha mfalme halikutupasa kwanza sisi? Lakini maneno yao Wayuda yalikuwa magumu kuliko yao Waisiraeli.