The chat will start when you send the first message.
1Wakati huo Bwana akaniambia: Jichongee mbao mbili za mawe kama zile za kwanza! Kisha panda kwangu huku mlimani! Jitengenezee nalo sanduku la mti![#2 Mose 25:10; 34:1.]
2Kisha nitaziandika hizo mbao yale maneno yaliyokuwa yameandikwa katika zile mbao za kwanza, ulizozivunja, kisha uziweke sandukuni.[#2 Mose 32:19.]
3Ndipo, nilipotengeneza sanduku la mti wa mgunga, nikachonga mbao mbili za mawe kama zile za kwanza, kisha nikapanda mlimani nikizishika hizo mbao mbili mkononi mwangu.
4Akaziandika hizo mbao kuwa kama mwandiko wa kwanza yale maneno kumi, Bwana aliyowaambia ninyi huko mlimani toka motoni siku hiyo, mlipokusanyika; kisha Bwana akanipa.[#5 Mose 9:10.]
5Ndipo, nilipogeuka, nikatelemka mlimani, nikaziweka hizo mbao katika sanduku, nililolitengeneza, zikakaa humo, kama Bwana alivyoniagiza.
6Kisha wana wa Isiraeli wakaondoka visimani kwa wana wa Yakani, wakaenda Mosera; ndiko, Haroni alikokufa, akazikwa huko, naye mwanawe Elazari akawa mtambikaji mahali pake.[#4 Mose 20:28; 33:32-33.]
7Walipoondoka huko wakaenda Gudigoda, tena toka Gudigoda, wakaenda Yotibata, ndiyo nchi yenye vijito vya maji.
8Siku zile Bwana akalitenga shina la Lawi, walichukue Sanduku la Agano la Bwana, tena wasimame mbele ya Bwana kumtumikia na kubariki watu kwa Jina lake, kama wanavyofanya hata leo.[#5 Mose 18:5,7; 4 Mose 6:23-27.]
9Kwa hiyo lawi asipate kwa ndugu zake fungu la nchi kuwa lake, kwani Bwana ndiye fungu lake mwenyewe, kama Bwana Mungu wako alivyosema.[#4 Mose 18:20.]
10Mimi niliposimama huko mlimani kama siku zile za kwanza siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, Bwana akanisikia hata mara hiyo, Bwana hakutaka kuwaangamiza ninyi,[#5 Mose 9:9.]
11kwa hiyo Bwana akaniambia: Inuka, uende na kuwatangulia watu, waiingie hiyo nchi kuichukua, iwe yao, kwani ndiyo, niliyowaapia baba zao kuwapa.
12Sasa, Isiraeli, yako mambo gani, Bwana Mungu wako anayokutakia, isipokuwa kumcha Bwana Mungu wako na kuzishika njia zake zote na kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote[#Mika 6:8.]
13na kuyashika maagizo ya Bwana na maongozi yake, mimi ninayokuagiza leo, upate kuona mema?
14Tazama, mbingu nazo mbingu za mbingu nayo nchi pamoja nayo yote yaliyomo ni yake Bwana.
15lakini Bwana alishikamana na baba zenu tu kwa kuwapenda, akawachagua ninyi mlio wazao wao waliokuwako nyuma yao akiwatoa katika makabila yote, kama inavyoelekea leo.[#5 Mose 7:6.]
16Kwa hiyo itahirini mioyo yenu, tena msizishupaze kosi zenu![#5 Mose 30:6.]
17kwani Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu, ni Bwana wa mabwana, ni Mungu mkubwa atishaye kwa matendo ya nguvu, hapendelei uso wa mtu, hachukui mapenyezo.
18Huamulia waliofiwa na wazazi nao wajane, hupenda wageni, awape chakula na nguo.
19Kwa hiyo nanyi wapendeni wageni, kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.[#2 Mose 22:21-24.]
20Mwogope Bwana Mungu wako, umtumikie, ugandamane naye. Napo utakapoapa litaje Jina lake!
21Yeye ni shangilio lako na Mungu wako aliyekufanyizia yale matendo makuu yaliyotisha, uliyoyaona kwa macho yako.
22Baba zako waliposhukia Misri walikuwa watu 70, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.[#5 Mose 1:10; 1 Mose 46:27.]