The chat will start when you send the first message.
1Bwana Mungu wako usimchinjie ng'ombe wala kondoo mwenye kilema au kibaya cho chote! Kwani hayo humchukiza Bwana Mungu wako.[#3 Mose 22:20.]
2Itakuwa, malangoni mwako miongoni mwa miji, Bwana Mungu wako atakayokupa, aonekane mtu mume au mke anayefanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wako kwa kupitana na Agano lake[#5 Mose 13:6-11.]
3akienda kutumikia miungu mingine na kuitambikia, kama ni jua au mwezi au vikosi vyote vya mbinguni, nisivyokuagiza.[#5 Mose 4:19.]
4Nawe utakapopashwa habari hizi au utakapovisikia tu, sharti utafute vema; kisha utakapoona, ya kuwa neno hilo ni kweli, ikaelekea, ya kama hilo tapisho limefanyika kweli kwao Waisiraeli,
5huna budi kumtoa malangoni pako huyo mtu mume au mke aliyelifanya hilo neno baya, kisha sharti mmpige mawe huyo mtu mume au mke, hata afe.
6Kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu mtu apaswaye na kufa ataweza kuuawa, lakini kwa ushahidi wa mtu mmoja mtu asiuawe![#4 Mose 35:30; Ebr. 10:28.]
7Mikono yao mashahidi sharti iwe ya kwanza ya kumwua, kisha mikono yao watu wote na ifuate; hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
8Itakapokuwa, shauri liwe gumu zaidi la kukushinda, kama wanastakiana manza za damu au unyang'anyi au mapigano au magomvi ya malangoni pako, basi, utainuka, upande kwenda mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua.
9Utakapofika kwa watambikaji Walawi na kwa mwamuzi atakayekuwako siku hizo uwaulize, nao watakukatia shauri hilo.[#2 Mambo 19:8,11.]
10Nawe sharti uyafanye, watakayokuambia na kukuonyesha njia mahali pale, Bwana atakapopachagua, nawe uangalie, uyafanye yote kuwa sawasawa, kama walivyokufunza.
11Sharti uyafuate hayo maonyo, watakayokufunza, nayo maamuzi, watakayokuambia, uyafanye hayo maneno, watakayokuonyesha, usiyaache kabisa kwenda kuumeni wala kushotoni.[#5 Mose 17:20.]
12Itakapokuwa, mtu ajikuze, akatae kumsikia mtambikaji anayesimama huko na kumtumikia Bwana Mungu wako au mwamuzi, huyo mtu hana budi kufa; ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo kwao Waisiraeli.
13Ndipo, watu wote watakaovisikia watakapoogopa, wasijikuze tena.
14Utakapoingia katika nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako, ukae huko, ndipo, utakaposema: Na nijiwekee mfalme, kama mataifa yote yanayokaa na kunizunguka pande zote yalivyo na wafalme.[#1 Sam. 8:5-6.]
15Napo hapo na umweke yule kuwa mfalme wako, Bwana Mungu wako atakayemchagua katikati ya ndugu zako; yeye ndiye, utakayemweka kuwa mfalme; mtu mgeni asiye ndugu yako hutaweza kumweka kuwa mkuu wako.
16Lakini angalia, asijitunzie farasi wengi, asiwarudishe watu hawa huko Misri kwa kuwa na farasi wengi, kwani Bwana aliwaambia: Msirudi tena huko na kuishika njia hii![#1 Fal. 10:25,28.]
17Wala asijipatie wanawake wengi, moyo wake usirudi nyuma! Wala asijiwekee fedha nyingi sana![#1 Fal. 11:4.]
18Lakini hapo, atakapokaa katika kiti chake cha kifalme, sharti ajiandikie mwandiko wa pili wa haya Maonyo katika kitabu na kukifuata kile cha watambikaji Walawi.[#2 Fal. 11:12.]
19Hicho kitabu sharti awe nacho, akisome siku zote za maisha yake, kusudi ajifundishe kumcha Bwana Mungu wake na kuyaangalia maneno yote ya haya Maonyo nayo ya haya maongozi, ayafanye.
20Asijikweze moyoni mwake kuwa mkuu kuliko ndugu zake, wala asiliache hili agizo kwenda wala kuumeni wala kushotoni, siku zake za kuwa mfalme yeye na wanawe katikati ya Waisiraeli zipate kuwa nyingi.[#5 Mose 5:32.]