The chat will start when you send the first message.
1Mfalme akaja pamoja na Hamani karamuni kwake Esteri, mkewe mfalme.[#Est. 5:8; 6:14.]
2Walipokunywa mvinyo, mfalme akamwuliza Esteri nayo siku hiyo ya pili: Unaomba nini, Esteri, mkewe mfalme? Utapewa. Unataka nini? Ingawa ni nusu ya ufalme, itafanyika.
3Ndipo, Esteri, mkewe mfalme, alipomjibu akisema: Kama nimeona upendeleo mbele yako, mfalme, navyo vikiwa vema kwako, mfalme, nipewe roho yangu kwa kuomba kwangu! Tena nipewe wenzangu wa ukoo kwa kutaka kwangu!
4Kwani tumekwisha kuuzwa mimi na wenzangu wa ukoo, tutoweshwe kwa kuuawa na kwa kuangamizwa. Kama tungaliuzwa tu kuwa watumwa na vijakazi, ningalinyamaza; lakini mpingani huyo hawezi kuvilipa, mfalme akipotelewa na watu hao.
5Mfalme Ahaswerosi akamwuliza Esteri, mkewe mfalme, na kusema: Ni nani huyu, tena yuko wapi aliyeushupaza moyo wake, upate kuwaza tendo kama hilo?
6Esteri akamwambia: Mtu wetu mpingani na adui ni huyu Hamani, ni mbaya. Ndipo, Hamani alipostuka mbele ya mfalme na mkewe mfalme.
7Lakini mfalme akainuka kwa makali hapo penye mvinyo, akaja bustanini kwenye jumba lake. Naye Hamani akasimama kumwomba Esteri, mkewe mfalme, amponye, kwani ameona, ya kuwa liko shauri baya, alilokwisha kukatiwa na mfalme.
8Mfalme alipotoka kule bustanini kwenye jumba lake na kuingia tena mle nyumbani, waliomkunywa mvinyo, Hamani alikuwa ameanguka penye kitanda, Esteri alipokaa; ndipo, mfalme aliposema: Je, Naye mkewe mfalme anataka kumkorofisha humu nyumbani mwangu? Neno hili lilipotoka kinywani mwa mfalme, ndipo, walipoufunika uso wa Hamani.
9Harbona, mmoja wao watumishi wa nyumbani waliomtumikia mfalme, akasema: Tazameni, ule mti, Hamani aliomsimikia Mordekai aliyesema mema ya kumponya mfalme, ungaliko kwenye nyumba ya Hamani, ni ule mrefu wa mikono hamsini. Ndipo, mfalme aliposema: Haya! Mtundikeni mumo humo!
10Wakamtundika Hamani katika ule mti, aliomsimikia Mordekai; kisha makali ya mfalme yakatulia.