The chat will start when you send the first message.
1Akaniambia: Wewe mwana wa mtu, simama kwa miguu yako, niseme na wewe!
2Aliposema na mimi, roho ikanijia, ikanipa kusimama kwa miguu yangu, nikamsikia aliyesema na mimi.
3Akaniambia: Wewe mwana wa mtu, mimi ninakutuma kwa wana wa Isiraeli walio mataifa makatavu, walionikataa mimi, wao wenyewe na baba zao wamenikosea mpaka leo.
4Hawa wana nao ni wenye nyuso zishupaazo na wenye mioyo migumu. Sasa mimi ninakutuma kwao, uwaambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema!
5Nao ikiwa wanasikia, au ikiwa wanaacha kusikia, kwani ndio mlango mkatavu, lakini watajua, ya kuwa yuko mfumbuaji katikati yao.[#Ez. 3:11,27.]
6Nawe mwana wa mtu, usiwaogope! Wala maneno yao usiyaogope! Ijapo miiba ikuchome, ijapo ukae penye nge, usiyaogope maneno yao! Wala usizistuke nyuso zao! Kwani ndio mlango mkatavu.
7Sharti uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikia, au ikiwa wanaacha kusikia, kwani ndio wakatavu.
8Nawe mwana wa mtu, yasikie, mimi ninayokuambia! Usiwe mkatavu kama mlango huu mkatavu! Kifumbue kinywa chako, ule, mimi nitakachokupa!
9Nilipotazama nikaona mkono nilionyosewa mimi, namo mwake nikaona kitabu kilichozingwa.[#Ufu. 10:8-11.]
10Akakizingua, nacho kilikuwa kimeandikwa upande wa mbele na wa nyuma; nayo yaliyoandikwa humo yalikuwa maombolezo na masikitiko na vilio.