The chat will start when you send the first message.
1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, fumbua yatakayokuwa, ukisema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Pigeni vilio kwamba: Ni siku gani hii?
3Kwani siku iko karibu, kweli siku ya Bwana iko karibu! ni siku yenye mawingu, itakuwa wakati wa wamizimu.[#Yoe. 1:15.]
4Panga zitaingia Misri, nayo nchi ya Nubi itatetemeka, watu waliopigwa kwa panga wakianguka huko Misri, wengine wakizichukua mali zao, tena wakiibomoa misingi yao.
5Wanubi na Waputi na Waludi nao wote waliochanganyika nao na Wakubu na wenyeji wa nchi, waliofanya maagano nao, wote pia watauawa kwa panga.
6Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nao walioiegemea nchi ya Misri wataangushwa, majivuno ya nguvu zake yakinyenyekezwa; kuanzia Migidoli kufikisha Siwene watauawa kwao kwa panga; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
7Nchi zao zitakuwa peke yao katikati ya nchi nyingine zilizo peke yao nazo, nayo miji yao itakuwa vivyo hivyo katikati ya miji iliyo mabomoko tu.
8Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana; nitakapowasha moto katika Misri, nao wasaidiaji wake wote watavunjwa.
9Siku ile watatoka kwangu wajumbe kwenda katika merikebu kuwastusha nao Wanubi wakaao na kutulia; ndipo, watakapotetemeka, ile siku ya Misri itakapokuja, kwani wataiona, inavyokuja.[#Yes. 18:2; 20:3-4.]
10Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitawakomesha wale watu wengi wa Misri kwa mkono wa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli.
11Yeye na watu wake, alio nao, ni wakali kuliko mataifa mengine; watapelekwa kuiangamiza hiyo nchi, watazichomoa panga zao kuwapiga Wamisri, waijaze hiyo nchi watu walioumizwa na panga.
12Nayo majito yake nitayakausha, nayo nchi hiyo nitaiuza mikononi mwa watu wabaya, niiangamize kwa mikono ya wageni pamoja nayo yote yaliyomo. Mimi Bwana nimeyasema.
13Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitayapoteza magogo ya kutambikia mle Nofu, hata vinyago nitavikomesha, pasiwe tena mkuu atokaye katika nchi ya Misri, tena nitaitisha nchi ya Misri.
14Patirosi nitaigeuza kuwa mapori tu, mle Soani nitawasha moto, namo No nitawahukumu waliomo.
15Mji wa Sini ulio boma lake Misri nitaumwagia makali yangu yenye moto, nao watu wengi waliomo No nitawaangamiza.
16Nitawasha moto katika Misri: Sini utaona machungu makuu, No utavunjwa kwa kubomolewa, Nofu utapata wanaousonga mchana.
17Vijana wa Oni na wa Pi-Beseti watauawa kwa panga, watu wao wengine watatekwa na kuhamishwa.
18Namo Tehafunesi mchana utageuka kuwa giza, nitakapozivunja mle bakora za kifalme za Misri; namo ndimo, nitakamoyakomesha majivuno ya nguvu zao; mji wenyewe wingu litaufunika, navyo vijiji vyake vya shambani vitatekwa na kuhamishwa.
19Hivyo ndivyo, nitakavyokata mashauri huko Misri; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
20Ikawa katika mwaka wa 11 siku ya saba ya mwezi wa kwanza, ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
21Mwana wa mtu, mkono wa Farao, mfalme wa Misri, nimeuvunja, lakini tazama, haukufungwa, upate kupona, hawakuutakia kitambaa tu, kwamba waufunge, wautie nguvu tena, upate kushika upanga.
22Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikimjia Farao, mfalme wa Misri, nitaivunja mikono yake, ule ulio na nguvu bado nao ule uliokwisha kuvunjika, niuangushe upanga chini uliomo mkononi mwake.
23Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika hizo nchi.
24Lakini mikono ya mfalme wa Babeli nitaitia nguvu, nao upanga wangu nitampa mkononi mwake, niivunje mikono ya Farao, ampigie yeye kite kama mtu mwenye vidonda.[#Ez. 29:20.]
25Mikono ya mfalme wa Babeli nitaitia nguvu, lakini mikono ya Farao itaanguka; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapompa mfalme wa Babeli upanga wangu mkononi mwake, aichomolee nchi ya Misri.
26Nao Wamisri nitawatawanya kwenye mataifa mengine na kuwatupatupa katika hizo nchi. Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.