The chat will start when you send the first message.
1Nawe mwana wa mtu, mfumbulie Gogi yatakayompata na kusema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Utaniona, nikikujia, Gogi uliye mkuu wa Rosi na wa Meseki na wa Tubali![#Ez. 38:2.]
2Nitakugeuza na kukushika kwa kamba, nikutoe huko kaskazini mbali na kukupandisha, uende, mpaka nikufikishe kwenye milima ya Isiraeli.
3Nitakupiga, upindi wako uanguke mkononi mwako mwa kushoto, nayo mishale yako nitaiangusha mkononi mwako mwa kuume.
4Milimani kwa Waisiraeli utaanguka wewe na vikosi vyako vyote nayo makabila, uliyo nayo; nitakutoa, uliwe nao ngusu na wote wenye mabawa na nyama wa porini.[#Ez. 39:17.]
5Utaanguka penye mapori, kwani mimi nimeyasema; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
6Nayo nchi ya Magogi nitaitupia moto nao wakaao salama katika visiwa; ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana.
7Lakini Jina langu takatifu watalijulisha kwao walio ukoo wangu wa Isiraeli, nami sitanyamaza tena, Jina langu takatifu likipatiwa uchafu; ndipo, wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana aliye Mtakatifu kwao Waisiraeli.
8Ndivyo, asemavyo Bwana: Hayo mtayaona, yakija kutimia siku ileile, niliyoisema.
9Ndipo, wakaao katika miji ya Waisiraeli watakapotoka, wavitumie vile vyombo vya vita kuwa kuni za kuwasha moto, zile ngao ndogo na kubwa, nazo pindi na mishale, nazo rungu na mikuki, wataitumia kuwa kuni za moto miaka saba.[#Sh. 46:10.]
10Hawataokota kuni za moto mashambani, wala hawatazikata misituni, kwani vyombo vya vita vitakuwa kuni zao. Hivyo watateka vitu kwao walioviteka vitu vyao na kuwanyang'anya mali zao; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
11Siku hiyo nitampa Gogi mahali pa kaburi kwao Waisiraeli katika bonde la wapitaji lililoko upande wa maawioni kwa jua kwenye bahari, nayo makaburi hayo yatawakinga wapitaji; ndiko, watakakomzika Gogi nao watu wake waliokuwa wengi, kisha watapaita Bonde la Wingi wa Gogi.
12Nao wa mlango wa Isiraeli watawazika muda wa miezi saba, kusudi waondoe uchafu katika nchi hiyo.
13Nao watu wote wa nchi hiyo watakuwa wakizika; hivyo watajipatia jina la kuwasifu siku ile, nitakapojitukuza; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
14Kisha watachagua watu wa kushika kazi hiyo siku zote, watembee katika nchi, wawazike wapitaji wale waliosazwa juu ya nchi, wauondoe uchafu huo. Ile miezi saba itakapopita, ndipo, watakapochunguza,
15watembezi wakitembea katika hiyo nchi; napo hapo, watakapoona mifupa ya mtu, watapajenga kando yake kichuguu, mpaka wazishi wamzike katika Bonde la Wingi wa Gogi.
16Hata mji utakaokuwako utaitwa Hamona (Wingi wa Watu). Hivyo ndivyo, watakavyoundoa huo uchafu wa hiyo nchi.
17Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nawe mwana wa mtu, waambie ndege wote wenye mabawa nao nyama wote wa porini: Kusanyikeni! Njoni mkitoka pande zote, mkutane penye ng'ombe zangu za tambiko, nitakazowachinjia kuwa karamu kubwa ya nyama za tambiko milimani kwa Waisiraeli, mle nyama na kunywa damu![#Ufu. 19:17-18.]
18Mtakula nyama za wapiga vita wenye nguvu, mtakunywa damu za wakuu wa nchi, ndio madume ya kondoo na wana kondoo na mbuzi na ng'ombe, wote ni manono ya Basani.
19Mtakula mafuta, mshibe, mtakunywa damu, mlewe kwa hizo ng'ombe zangu za tambiko, nitakazowachinjia.
20Mtashiba mezani pangu kwa nyama za farasi nazo zao waliowapanda, kwa nyama za wapiga vita wenye nguvu nazo zao wote waliojiendea tu kupigana; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
21Ndivyo, nitakavyoutokeza utukufu wangu kwa wamizimu, nao wamizimu wote watayaona mapatilizo yangu, nitakayowapatia, nao mkono wangu, nilioutoa kuwakamata.
22Ndipo, walio mlango wa Isiraeli watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana Mungu wao, tangu siku ile hata siku zitakazokuja.
23Nao wamizimu watajua, ya kuwa walio mlango wa Isiraeli walihamishwa kwa ajili ya manza, walizokora walipoyavunja maagano yangu; kwa hiyo naliuficha uso wangu, wasiuone, nikawatia mikononi mwao waliowasonga, wao wote wauawe kwa panga.[#Yes. 54:8.]
24Hivyo, walivyojipatia uchafu kwa mapotovu yao, ndivyo, nilivyowafanyizia nilipouficha uso wangu, wasiuone.
25Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Sasa nitayafungua mafungo yake Yakobo, niwahurumie wote walio mlango wa Isiraeli kwa kutenda wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.[#Ez. 16:53-63.]
26Nao watashikwa na soni iwapasayo kwa hivyo, walivyoyavunja maagano yangu yote, watakapokaa salama katika nchi yao, kwani hatakuwako atakayewastusha.
27Nitakapowarudisha kwao na kuwatoa kwenye makabila mengine na kuwakusanya, wazitoke nchi za adui zao, ndipo, nitakapojitokeza kwao kuwa Mtakatifu machoni pa wamizimu wengi;
28nao watajua, ya kuwa mimi Bwana Mungu wao kweli naliwahamisha kwenda kwa wamizimu, lakini nitawakusanya tena, warudi katika nchi yao, sitasaza hata mmoja wao huko.
29Wala sitauficha uso wangu tena, wasiuone, kwani nitawamwagia walio mlango wa Isiraeli Roho yangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.[#Ez. 36:26-27; Yes. 44:3.]