Wagalatia 5

Wagalatia 5

Wakristo wasitahiriwe!

1*Kristo ametukomboa, tuwe waungwana. Kwa hiyo simameni, msijitie tena katika mafungo ya utumwa![#Gal. 4:5,8-11,31; Mar. 7:3-4; Tume. 15:10.]

2Tazameni, mimi Paulo nawaambiani: Kristo hatawafaa kitu, mkitahiriwa.

3Tena namshuhudia kila mtu aliyetahiriwa, ya kuwa ni mdeni wa kuyafanya Maonyo yote.

4Ninyi mtakao kupata wongofu kwa kuyafanya Maonyo mmetengwa na Kristo, mmeanguka na kuyaacha magawio.

5Kwani sisi kwa nguvu ya Roho twakishika kingojeo cha kwamba: Tutapata wongofu kwa kumtegemea Mungu.

6Maana tukiwa naye Kristo Yesu, kunakotupa nguvu siko kutahiriwa, wala kutotahiriwa, ila kumtegemea Mungu kutimilikako katika kupendana.[#Gal. 6:15; Rom. 2:26; 1 Kor. 7:19.]

7Mlianza kushika njia nzuri; yuko nani aliyewakwaza, msiyatii yaliyo ya kweli?

8Kazi hii ya kuwavutavuta hivyo haikutoka kwake yeye aliyewaita.[#Gal. 1:6.]

9Chachu kidogo hulichachusha donge lote.[#1 Kor. 5:6.]

10Hivyo, mlivyo naye Bwana, mimi huwawazia kuwa welekevu kwamba: Hamtaigeuza mioyo. Lakini aliyewahangaisha hivyo ataiona hukumu yake, awaye yote.[#Gal. 1:7; 2 Kor. 11:15.]

11Lakini mimi, ndugu, kama ningetangaza hata sasa, watu watahiriwe, ningekuwa mwenye kufukuzwa? Nayo makwazo ya msalaba yangekuwa yameondolewa.[#Gal. 6:12; 1 Kor. 1:23.]

12Ingefaa, wale wenye kuwatukusa wakatwe na kutengwa.[#Sh. 12:4.]

Matendo ya mwili nayo matendo ya Roho.

13Ndugu, ninyi mliitiwa kuwa waungwana. Lakini uungwana huo msiugeuze kuwa tokeo la tamaa za miili yenu, ila mtumikiane na kupendana!

14Kwani Maonyo yote hutimilika katika neno moja, ndilo hili:

Umpende mwenzio,

kama unavyojipenda mwenyewe!

15Lakini mkiumana, mkilana ninyi kwa ninyi, angalieni, msimezwe kabisa kwa kule kulana.*

16*Lakini nasema, mwendelee Kiroho! Hivyo hamtaweza kuzitimiza tamaa za miili.[#Gal. 5:25.]

17Kwani miili huyatamani yanayokataliwa na Roho, naye Roho huyatamani yanayokataliwa na miili; hawa wawili hupingana, msipate kuyafanya, myatakayo.[#Rom. 7:15,23.]

18Lakini mkiongozwa na Roho ham tena watumwa wa Maonyo.

19Nayo matendo ya miili yako waziwazi, ndiyo ugoni, uchafu, uasherati,[#1 Kor. 6:9-10.]

20kutambikia vinyago, uchawi, uchukivu, ugomvi, wivu, mifundo ya mioyo, machokozi, matengano, vyama,

21kijicho, ulevi, ulafi, nayo mambo mengine yaliyofanana nayo. Kama nilivyowaambia kale, vivyo hivyo nawaambia tena: Wafanyizao mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.[#Ef. 5:5; Ufu. 22:15.]

22Lakini mazao ya Roho ndiyo haya: upendano, furaha, utengemano, uvumilivu, utu, wema, welekevu,[#Ef. 5:9.]

23utulivu, kuzishinda tamaa. Mambo kama hayo hayakataliwi na Maonyo.[#1 Tim. 1:9.]

24Lakini wa Kristo Yesu huiua miili na kuiwamba msalabani pamoja na mawazo mabaya na tamaa.*[#Rom. 6:6; 8:9; Kol. 3:5.]

Kusaidiana na kupokeana.

25*Tukiwa wa Kiroho na tuendelee Kiroho![#Gal. 5:16; Rom. 8:4.]

26Tusitafute utukufu ulio wa bure, tukichokozana, tena tukioneana kijicho![#Fil. 2:3.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania