The chat will start when you send the first message.
1Bwana akaniambia: Nenda tena kumpenda mwanamke mzinzi anayependwa na mwingine, kama Bwana anavyowapenda wana wa Isiraeli, nao huigeukia miungu mingine kwa kuyapenda maandazi ya zabibu.[#Hos. 1:2.]
2Nikamnunua, awe wangu, nikatoa fedha kumi na tano na frasila kumi na tano za mawele.
3Nikamwambia: Siku nyingi utakaa tu kwangu, usizini, wala usiwe wa mume; mimi nami nitakuwa vivyo hivyo kwako.
4Kwani wana wa Isiraeli watakaa siku nyingi pasipo mfalme wala mkuu, pasipo tambiko wala kinyago, pasipo vazi la mtambikaji wala Patakatifu.[#2 Mambo 15:3.]
5Kisha wana wa Isiraeli watarudi, wamtafute Bwana Mungu wao na Dawidi, mfalme wao; siku zitakazokuwa za mwisho watamwendea Bwana na wema wake kwa kutetemeka.[#Yer. 30:9,21-22; Ez. 34:23-24.]