The chat will start when you send the first message.
1Maneno kama haya nimeyasikia mara nyingi,
2ninyi nyote mwatuliza moyo na kuusumbua!
3Maneno yaliyo kama upepo yamekwisha? Au kuna nini kinachokuchochea, ukinijibu hivyo?
4Mimi nami ningeweza kusema kama ninyi; kama roho zenu zingekuwa mahali pake roho yangu, nami ningeweza kukusanya maneno mazuri ya kuwaambia pamoja na kuwatingishia kichwa changu.[#Sh. 22:8.]
5Lakini kwa maneno ya kinywa changu ningewatia nguvu, nayo midomo yangu ingewatuliza mioyo kwa kuwakingia maovu.
6Lakini maumivu yangu hayazuiliki, ijapo niseme; tena kuna nini ninayopungukiwa, nikiacha kusema?
7Kwa kuuangamiza mlango wangu wote amenichokesha sasa.
8Wewe ukanikunjamanisha, upate ushahidi wa kunishinda, nako kukonda kwangu kwaniinukia, kunisute usoni pangu.
9Ukali wake ukaninyafua kwa kunionea tu, nayo meno yake huyatumia ya kunikerezea, akanikazia macho yake makali, yeye mpingani wangu.[#Sh. 35:16; 112:10.]
10Wako wanaoniasamia vinywa vyao, wakanipiga mashavu na kunitukana, wote pia wakakusanyika kunijia mimi.[#Sh. 22:8.]
11Mungu akanifunga, kisha akanitoa, wao wanipotoe, akanitia mikononi mwao wasiomcha.
12Nalikaa na kutengemana, mara akaniponda, akanikamata shingoni, akanibwaga mwambani, kisha akanisimamisha tena, niwe shabaha yake.[#Omb. 3:12.]
13Wapigaji wake wa mishale wakanizunguka, wakanipasua mafigo yangu pasipo huruma, nayo maji yangu ya nyongo wakayamwaga chini.
14Kwa kunitia kidonda kwa kidonda akaniumiza vibaya, kama fundi wa vita akanijia na kupiga mbio sana.
15Gunia la kuifunika ngozi ya mwili wangu ndilo, nililojishonea, nayo pembe yangu nikaichomeka uvumbini.[#1 Mose 37:34.]
16Uso wangu ukaiva sana kwa kulia, napo penye kope zangu kiko kivuli kama cha kifo.
17Tena mikononi mwangu hamna ukorofi, nayo maombo yangu hutakata.
18Usiifunike damu yangu, wewe nchi, wala malalamiko yangu yasipate kituo![#1 Mose 4:10.]
19Jueni: Hata sasa yuko shahidi wangu kule mbinguni, huko juu yuko atakayenitetea.
20Rafiki zangu wananifyoza, lakini macho yangu hivyo, yanavyojaa machozi, humtazamia Mungu.[#Omb. 3:14.]
21Yeye Mungu amwamulie mtu, ijapo ashindane naye, hata mwana wa Adamu akishindana na mwenzake, amkatie shauri.
22Kwani miaka imekwisha hesabiwa itakayokuja; nayo itakapokwisha, sina budi kuishika ile njia isiyo na kurudi.[#Iy. 10:21.]