Yosua 19

Yosua 19

Fungu la shina la Simeoni.

1Kura ya pili iliyotokea ilikuwa ya shina la wana wa Simeoni ya kuzigawanyia koo zao; nalo fungu lao lilikuwa katikati ya wana wa Yuda.

2Hilo fungu, walilolipata, liwe lao, lilikuwa: Beri-Seba na Seba na Molada,

3na Hasari-Suali na Bala na Esemu,

4na Eltoladi na Betuli na Horma,

5na Siklagi na Beti-Markaboti na Hasari-Susa,

6na Beti-Lebaoti na Saruheni; ndio miji 13 na mitaa yao.

7Aini, Rimoni na Eteri na Asani, ndio miji 4 na mitaa yao.

8Tena mitaa yote pia iliyoizunguka miji hii mpaka Bala-Beri ulio Rama wa kusini. Hii lilikuwa fungu lao wana wa Simeoni la kuzigawanyia koo zao.

9Hili fungu la wana wa Simeoni lilichukuliwa katika nchi, wana wa Yuda waliyopimiwa, kwani fungu lao wana wa Yuda lilikuwa kubwa zaidi, wasilikae lote. Kwa hiyo wana wa Simeoni walipata fungu lao katikati ya fungu lao wale.

Fungu la shiria la Zebuluni.

10Kura ya tatu iliyotokea ilikuwa ya wana wa Zebuluni ya kuzigawanyia koo zao, nao mpaka wa fungu lao ulifika hata Saridi.

11Toka huko mpaka wao ulipanda upande wa baharini kufika Marala na kugusa Dabeseti, kisha ulikigusa kijito kile kinachopita mbele ya Yokinamu.

12Tena toka Saridi mpaka uligeukia upande wa mashariki, ndio maawioni kwa jua, ufike kwenye mpaka wa Kisiloti-Tabori, toka huko ulifika Daberati na kupanda Yafia.

13Toka huko uliendelea upande wa mashariki, ndio wa maawioni, ufike Gati-Heferi na Eti-Kasini, utokee Rimoni na kufika hata Nea.

14Kisha mpaka uliuzunguka mji huu upande wa kaskazini wa Hanatoni, upate kutokea bondeni kwa Ifuta-Eli,

15kuliko na miji ya Katati na Nahalali na Simuroni na Idala na Beti-Lehemu; miji ilikuwa 12 na mitaa yao.[#Amu. 1:30.]

16Hili lilikuwa fungu lao wana wa Zebuluni la kuzigawanyia koo zao ile miji pamoja na mitaa yao.

Fungu la shina la Isakari.

17Kura ya nne iliyotokea ilikuwa ya wana wa Isakari ya kuzigawanyia koo zao.

18Mpaka wao ulichukua Izireeli na Kesuloti na Sunemu,

19na Hafaraimu na Sioni na Anaharati,[#2 Fal. 4:8.]

20na Rabiti na Kisioni na Abesi,

21na Remeti na Eni-Ganimu na Eni-Hada na Beti-Pasesi.

22Kisha mpaka uligusa Tabori na Sahasima na Beti-Semesi, kisha mpaka wao ulitokea Yordani; miji ilikuwa 16 pamoja na mitaa yao.

23Hili lilikuwa fungu la shina la wana wa Isakari la kuzigawanyia koo zao ile miji pamoja na mitaa yao.

Fungu la shina la Aseri.

24Kura ya tano iliyotokea ilikuwa ya shina la wana wa Aseri ya kuzigawanyia koo zao.

25Mpaka wao ulichukua Helkati na Hali na Beteni na Akisafu,

26na Alameleki na Amadi na Misali; kisha mpaka uligusa Karmeli upande wa baharini na Sihori-Libunati.

27Toka huko mpaka uligeukia upande wa maawioni kwa jua kufika Beti-Dagoni, kisha uligusa Zebuluni na bonde la Ifuta-Eli upande wake wa kaskazini, ulipita Beti-Emeki na Nieli, upate kutokea Kabuli kushotoni kwake.

28Kisha ulichukua Eburoni na Rehobu na Hamoni na Kana, uufikie ule mji mkubwa wa Sidoni.

29Huko mpaka uligeuka tena kufika Rama, hata mji wa Tiro uliokuwa na boma, kisha mpaka uligeuka tena kufika Hosa, upate kutokea baharini upande wa nchi ya Akizibu.[#Yos. 15:44; Amu. 1:31.]

30Hata Uma na Afeki na Rehobu ilikuwa ya huko. Miji ilikuwa 22 pamoja na mitaa yao.

31Hili lilikuwa fungu la shina la wana wa Aseri la kuzigawanyia koo zao ile miji pamoja na mitaa yao.

Fungu la shina la Nafutali.

32Kura ya sita iliyotokea ilikuwa ya wana wa Nafutali ya kuzigawanyia koo zao.

33Mpaka wao ulitoka Helefu kwenye mvule wa Sananimu, ulichukua Adami-Nekebu na Yabuneli, hata Lakumu, utokee Yordani.

34Tena mpaka uligeukia upande wa baharini, ufike Azinoti-Tabori; ulipotoka huko ulikwenda Hukoki, upande wa kusini uligusa Zebuluni, nao upande wa baharini uligusa Aseri, nao upande wa maawioni kwa jua uligusa Yuda kwenye Yordani.

35Miji yenye maboma ilikuwa: Sidimu, Seri na Hamati, Rakati na Kinereti (Genezareti),

36na Adama na Rama na Hasori,

37na Kedesi na Edirei na Eni-Hasori,

38na Ironi na Migidali-Eli, Horemu na Beti-Anati na Beti-Semesi; miji ilikuwa 19 pamoja na mitaa yao.[#Amu. 1:33.]

39Hili lilikuwa fungu la shina la wana wa Nafutali la Kuzigawanyia koo zao ile miji pamoja na mitaa yao.

Fungu la shina la Dani.

40Kura ya saba iliyotokea ya shina la wana wa Dani ya kuzigawanyia koo zao.

41Mpaka wa fungu lao ulichukua Sora na Estaoli na Iri-Semesi,

42na Salabini na Ayaloni na Itila,

43na Eloni na Timuna na Ekroni,[#Amu. 1:35.]

44na Elteke na Gibetoni na Bala,

45na Yudi na Bene-Beraki na Gati-Rimoni,

46na Me-arkoni na Rakoni nayo nchi ielekeayo Yafo;[#Yona 1:3.]

47huko ndiko, mpaka wa wana wa Dani ulikotokea. Halafu wana wa Dani walikwenda kupigana na mji wa Lesemu, wakauteka, wakawapiga waliokuwamo kwa ukali wa panga, kisha wakauchukua, wakakaa humo, wakaacha kuuita Lesemu wakauita Dani kwa jina la baba yao Dani.[#Amu. 18:27,29.]

48Hili lilikuwa fungu la shina la wana wa Dani la kuzigawanyia koo zao ile miji pamoja na mitaa yao.

Fungu lake Yosua.

49Wana wa Isiraeli walipokwisha kuigawanya nchi hii na kujipatia mafungu yao katika mipaka yake wakampa Yosua, mwana wa Nuni, fungu lake katikati yao.

50Kwa kuagizwa na Bwana wakampa huo mji, alioutaka, ndio Timunati-Sera milimani kwa Efuraimu, kisha akaujenga mji huu, akakaa humo.[#Yos. 24:30.]

51Haya ndiyo mafungu, mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, na wakuu wa milango ya baba zao waliyowagawanyia mashina ya wana wa Isiraeli kwa kuyapigia kura huko Silo machoni pa Bwana pa kuliingilia Hema la Mkutano; ndivyo, walivyomaliza kuigawanya nchi hii.[#Yos. 14:1; 18:1.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania