The chat will start when you send the first message.
1Nikasema: Sikilizeni, ninyi mlio vichwa vyao wa Yakobo,
ninyi mlio wakuu wa mlango wa Isiraeli!
Je? Haiwapasi ninyi kujua, jinsi mashauri yanavyokatwa
sawasawa?
2Lakini ninyi huchukizwa nayo yaliyo mema,
mkapendezwa nayo yaliyo mabaya;
ninyi huchuna watu ngozi zao,
nazo nyama zao huziondoa mifupani kwao.
3Ninyi ndio mnaozila nyama zao walio ukoo wangu,
tena mkiisha kuwavua ngozi zao mwawavunja nayo mifupa
yao,
mkawakatakata vipande kama vya kuweka chunguni
au kama nyama zinazotiwa katika sufuria.
4Kwa hiyo hapo, watakapomlilia Bwana, hatawaitikia,
ila atauficha uso wake, usiwatazame wakati huo,
kama inavyowapasa kwa matendo yao mabaya, waliyoyafanya.
5Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya wafumbuaji
wanaowapoteza walio ukoo wangu,
ndio wanaotangaza kwamba: Tengemaneni tu!
wakipata vya kutafuna kwa meno yao,
lakini mtu asipowapa vya kutia vinywani mwao,
humpatia vita vya watakatifu
6Kwa hiyo usiku utawaguia, msione kitu,
na giza, msiweze kuagua,
nalo jua litawachwea wafumbuaji hao,
hata siku itakuwa yenye giza kwao.
7Ndipo, hao wachunguzaji watakapopatwa na soni,
nao waaguaji hao wataiva nyuso,
wao wote watajifunika ndevu zao za midomo,
kwa kuwa Mungu hawajibu kamwe.
8Lakini mimi nimejaa nguvu, nilizopewa na Roho ya Bwana,[#Yes. 58:1.]
nikapewa kumaliza mashauri kwa uwezo wa kushinda,
nipate kuwatangazia wa Yakobo mapotovu yao
nao Waisiraeli makosa yao.
9Sikilizeni, ninyi mlio vichwa vyao wa Yakobo,
nanyi mlio waamuzi wa mlango wa Isiraeli!
Mwachukizwa na mashauri yaliyo sawa,
nayo yote yanyokayo mwayapotoa!
10Sioni mwaujenga kwa damu nao Yerusalemu kwa mapotovu.[#Hab. 2:12.]
11Wakuu wao hukata mashauri kwa kupenyezewa mali,
nao watambikaji wao hufundisha kulipwa,
nao wafumbuaji wao hufumbua kwa kupata fedha,
tena hujiegemezea kwake Bwana na kusema:
Je? Bwana hayuko kwetu katikati?
Hakuna kibaya kitakachotupata.
12Kweli kwa ajili yenu ninyi Sioni utalimwa kuwa shamba,
nao Yerusalemu utageuka kuwa chungu la mabomoko,
nao mlima wenye Nyumba hii utageuka kuwa kilima chenye
mwitu.