The chat will start when you send the first message.
1Alipoingia tena katika nyumba ya kuombea, mle mlikuwa na mtu mwenye mkono uliokuwa umekaukiana.
2Wakamtunduia, kama atamponya siku ya mapumziko, wapate kumsuta.
3Akamwambia yule mwenye mkono uliokaukiana: Inuka, uje hapa katikati!
4Kisha akawauliza: Iko ruhusa siku ya mapumziko kufanya mema au kufanya maovu? kuponya roho ya mtu au kuiua? Waliponyamaza,
5ukali ukamjia, akawatazama waliokuwako, akausikitikia ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu: Unyoshe mkono wako! Alipounyosha, huo mkono wake ukageuka kuwa mzima.[#Yoh. 11:33.]
6Mafariseo wakatoka, papo hapo wao pamoja na watu wa Herode wakamlia njama ya kumwangamiza.[#Mar. 6:14; Mat. 22:16.]
7Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake kwenda upande wa baharini. Kundi la watu wengi sana waliotoka Galilea likamfuata. Tena wengi waliotoka Yudea
8na Yerusalemu na Idumea na ng'ambo ya Yordani na upande wa Tiro na Sidoni, wakamwendea, kwani waliyasikia yote, aliyoyafanya.[#Mat. 4:25.]
9Akawaambia wanafunzi wake, wamtengenezee chombo kidogo kwa ajili ya makundi ya watu, wasije kumsongasonga.
10Kwa kuwa aliponya wengi, wote walioteseka wakamwangukiaangukia, wapate kumgusa tu.
11Hata pepo wachafu, kila walipomwona, wakamwangukia wakipiga kelele wakisema: Wewe ndiwe Mwana wa Mungu![#Luk. 4:41.]
12Akawatisha sana, wasimtangaze.[#Mar. 1:34.]
13Kisha akapanda mlimani, akawaita, aliowataka mwenyewe; wakaja kwake.
14Akawaweka kumi na wawili, wawe pamoja naye, apate kuwatuma kupiga mbiu,
15wakiisha kupewa nguvu za kufukuza pepo.
16Akawaweka hao kumi na wawili: Simoni akampa jina la Petero.[#Yoh. 1:42.]
17Yakobo, mwana wa Zebedeo, na Yohana, nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, ni kwamba: Wana wa Ngurumo.[#Luk. 9:54.]
18Akawaweka nao akina Anderea na Filipo na Bartolomeo na Mateo na Toma na Yakobo, mwana wa Alfeo, na Tadeo na Simoni wa Kana
19na Yuda Iskariota aliyemchongea halafu.
20Alipoingia nyumbani, ndipo, kundi la watu lilipokusanyika tena, wenyewe wasiweze hata kula mkate.
21Lakini ndugu zake walipoyasikia wakatoka, waje kumchukua, kwa maana walisema: Amepatwa na kichaa.[#Yoh. 7:20; 8:48,52; 10:20.]
(22-30: Mat. 12:24-32; Luk. 11:15-22; 12:10.)22Nao waandishi waliokuwa wametelemka toka Yerusalemu walisema: Ana Belzebuli. Tena wakasema: Nguvu ya huyo mkuu wa pepo ndiyo, anayofukuzia pepo.
23Akawaita, akawaambia kwa mifano: Satani awezaje kumfukuza Satani mwenziwe?
24Ufalme unapogombana wao kwa wao, ufalme huo hausimamiki.
25Nayo nyumba inapogombana wao kwa wao, nyumba hiyo haitaweza kusimama.
26Naye Satani anapojiinukia mwenyewe na kujigombanisha hawezi kusimama, ila ataishiwa.
27Hakuna mtu awezaye kuingia katika nyumba ya mwenye nguvu, aviteke vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; kisha ataweza kuiteka nyumba yake.
28Kweli nawaambiani: Wana wa watu wataondolewa yote, hata maneno yote ya kumbeza Mungu.
29Lakini mtu atakayembeza Roho Mtakatifu hapati kuondolewa kale na kale, ila kosa lake litamkalia pasipo mwisho.
30Aliwaambia hivyo kwa vile walivyosema: Ana pepo mchafu.[#Mar. 3:22.]
31Kisha mama yake na ndugu zake wakaja, wakasimama nje, wakatuma mtu kwake, amwite.
32Kundi la watu likawamo likimzunguka, wakamwambia: Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.
33Akajibu akiwaambia: Aliye mama yangu ni nani? Ndugu zangu ni akina nani?
34Akawatazama waliokaa huko na huko, wakimzunguka pande zote, akasema: Watazameni walio mama yangu na ndugu zangu!
35Mtu ye yote atakayeyafanya, Mungu ayatakayo, huyo ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.