The chat will start when you send the first message.
1Siku ya kwanza ya mwezi wa saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi, iwe sikukuu yenu ya Shangwe.[#3 Mose 23:24-25.]
2Hapo na mtoe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza Bwana: dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
3Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume la ng'ombe na vibaba sita vya dume la kondoo,
4na vibaba vitatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
5Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo kuwapatia ninyi upozi.
6Hao na mtoe pamoja na ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima za mwandamo wa mwezi pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao vya tambiko, kama ilivyo desturi yao kuwa moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.
7Siku ya kumi ya mwezi huo wa saba na mkutanie Patakatifu na kujitesa kwa kufunga, msifanye kazi yo yote,[#3 Mose 23:27-32.]
8ila mtolee Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe mnuko wa kumpendeza: dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema; hawa ndio, mtakaowatoa.
9Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume la ng'ombe na vibaba sita vya dume moja la kondoo,
10na vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo saba.
11Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya weuo ya sikukuu ya Mapoza na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao ya tambiko.[#3 Mose 16:11-22.]
12Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi, ila mzile hizo sikukuu za Bwana siku saba.[#3 Mose 23:34-43.]
13Hapo na mtoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana: madume kumi na matatu ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
14Navyo vilaji vyao vya tambiko na viwe vibaba tisa vya unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta vya dume moja la ng'ombe wa wale madume ya ng'ombe kumi na matatu na vibaba sita vya dume moja la kondoo wa wale madume mawili ya kondoo,
15na vibaba vitatutatu vya kila mwana kondoo mmoja wa wale wana kondoo kumi na wanne.
16Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
17Siku ya pili na mtoe madume kumi na mawili ya ng'ombe walio vijana bado na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
18Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe navyo vya madume ya kondoo navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
19Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku pamoja na vilaji vyake vya tambiko, tena na mvitoe navyo vinywaji vyao vya tambiko.
20Siku ya tatu na mtoe madume kumi na moja ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
21Navyo vilaji na vinywaji vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
22Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambik ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
23Siku ya nne na mtoe madume kumi ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
24Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
25Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
26Siku ya tano na mtoe madume tisa ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
27Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
28Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
29Siku ya sita na mtoe madume manane ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana mbuzi kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
30Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
31Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
32Siku ya saba na mtoe madume saba ya ng'ombe na madume mawili ya kondoo na wana kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja wasio na kilema.
33Navyo vilaji na vinywaji vyao vya tambiko vya madume ya ng'ombe, navyo vya madume ya kondoo, navyo vya wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
34Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
35Siku ya nane na iwe ya mkutano mkuu kwenu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,
36ila mtoe ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, ziwe moto wenye mnuko wa kumpendeza Bwana: dume moja la ng'ombe na dume moja la kondoo na wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na kilema.
37Navyo vilaji na vinywaji vyote vya tambiko vya yule dume la ng'ombe, navyo vya yule dume la kondoo, navyo vya wale wana kondoo na mvitoe kwa hesabu yao kama desturi.
38Tena na mtoe dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo pamoja na ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima ya kila siku, tena na mvitoe navyo vilaji na vinywaji vyake vya tambiko.
39Hizo ndizo ng'ombe za tambiko, mtakazomtolea Bwana, sikukuu zenu zitakapotimia; tena ziko zile, mtakazozitoa kwa kuapa au kwa kupenda wenyewe kuwa ng'ombe zenu za tambiko za kuteketezwa nzima au vilaji au vinywaji vyenu vya tambiko au ng'ombe zenu za tambiko za shukrani.
40Mose akawaambia wana wa Isiraeli haya yote, kama Bwana alivyomwagiza Mose.