Mifano 2

Mifano 2

Mbaraka ya kutafuta ujuzi.

1*Mwanangu, ukiyapokea maneno yangu

na kuyashika maagizo yangu moyoni mwako,

2ukiutegea werevu wa kweli sikio lako,

ukauelekezea utambuzi moyo wako,

3ukiziita akili na kuipaza sauti yako, upate utambuzi,[#Yak. 1:5.]

4ukiutafuta, kama unavyotafuta fedha,

ukiuchunguza, kama unavyochunguza mali zilizofichwa:

5ndipo, utakapoitambua maana ya kumcha Bwana,

tena ndipo, utakapopata kumjua Mungu.

6Kwani Bwana huerevusha kweli,

kinywani mwake hutoka ujuzi na utambuzi.

7Wanyokao aliwawekea wokovu,

ni ngao yao waendeleao pasipo kukosa,

8ayalinde mapito yaliyo sawa

na kuzingalia njia zao wamchao.*

9Ndipo, utakapotambua wongofu na mashauri yaliyo sawa

nayo yanyokayo na kila njia njema,

10kwani werevu wa kweli utaingia moyoni mwako,

nao ujuzi utaupendeza roho yako.

11Mawazo mema ya moyo yatakuangalia,

nao utambuzi utakulinda,

12yakuponye, usiishike njia ya wabaya,

usiwafuate watu wasemao mapotovu,

13walioziacha njia zinyokazo,

waende katika njia zenye giza.

14Wanaofurahiwa na kufanya mabaya,

wanaoshangilia mapotovu ya wabaya,

15njia zao nazo ni za upotovu,

nayo mikondo yao hainyoki.

16Nayo yale mawazo mema ya moyo yatakuponya,

usimchukue mwanamke mgoni aliye wa mwingine,

ijapo akubembeleze kwa maneno mazuri;

17kwa kuwa alimwacha mpendwa wa ujana wake

na kulisahau agano la Mungu wake,

18nyumba yake inatumbukia penye kifo,

nayo mapito yake humwongoza kwenda kwao wazimu.

19Wote walioingia mwake hakuna atakayerudi,

wala hakuna atayezifikilia njia za kwenda uzimani.

20Huku na kwamba: Uende katika njia ya watu wema

na kuyashika mapito yao walio waongofu.

21Kwani wanyokao ndio watakaokaa katika nchi,

nao wamchao Mungu watasazwa huku;

22lakini wasiomcha Mungu watang'olewa katika nchi,

nao waliomwacha Bwana watapokonywa huku.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania