The chat will start when you send the first message.
1Usione wivu kwa ajili ya watu wabaya,
wala usitamani kuwa mwenzao!
2Kwani mioyo yao huwaza mwangamizo,
nayo midomo yao husema makorofi.
3Nyumba hujengwa kwa werevu wa kweli
ikishikizwa kwa utambuzi.
4Kwa ujuzi vyumba vyake hujazwa
vitu vyote vyenye kima vipendezavyo.
5Mtu mwerevu wa kweli ni mwenye nguvu,
naye mwenye ujuzi huzidisha uwezo.
6Kwani kwa kuzitumia akili utapiga vita,
wokovu nao huja kwa kupiga mashauri yaliyo mema.
7Werevu wa kweli humkalia mjinga juu sana, asiufikie,
hakifunui kinywa chake mlangoni penye mashauri.
8Awazaye kufanyia wengine mabaya tu
huitwa mtunga maovu.
9Mawazo ya mjinga ni ya ukosaji,
naye mfyozaji huwatapisha watu.
10Ukilegea siku ya kusongwa,
nguvu zako ni chache.
11Waponye wanaopelekwa kuuawa,
nao wanokumbwakumbwa kwenda kuchinjwa sharti uwaopoe!
12Ukisema: Hatukuyajua,
je? Yeye aijaribuye mioyo haitambui?
Je? Yeye ailindaye roho yako haijui?
Naye ndiye atakayemlipisha kila mtu matendo yake.
13Mwanangu, ule asali, kwani ni njema,
ile asali iliyo safi yenyewe, kwani ni tamu, ukiitia kinywani.
14*Nao werevu wa kweli uujue, ya kuwa ni utamu wa roho;
ukiupata, basi, mwisho utafanikiwa,
nacho kingojeo chako hakitang'oleka.
15Wewe usiyemcha Mungu, usiotee penye kao la mwongofu,
wala usipabomoe pake pa kulalia!
16Kwani mwongofu akianguka mara saba huinuka,
lakini wasiomcha Mungu hujikwaza penye mabaya.
17Mchukivu wako akianguka, usifurahi,
wala moyo wako usipige shangwe, akijikwaa.
18Bwana asivione, maana ni vibaya machoni pake,
akaacha kumtolea yule makali yake.
19Usijichafushe moyo kwa ajili yao watendao mabaya
wala usiwaonee wivu wasiomcha Mungu!
20Kwani mwisho wake mbaya hautakuwa mwema,
nazo taa zao wasiomcha Mungu huzimika.*
21Mwanangu, mwogope Bwana, hata mfalme!
Usifanye bia nao wanaoigeuzageuza mioyo!
22Kwani mara utatokea mwangamizo wao,
tena yuko nani ajuaye, mabaya yatakapowapata nyote wawili?
Upendeleo haufai kabisa shaurini.
24Amwambiaye mkosaji: Hukukosa,
ndiye, makabila ya watu watakayemwapiza,
koo zote watamtakia mabaya.
25Lakini wao wanaomchapa hupendeza,
mbaraka ya kuwapatia mema huwajia.
26Kama mwenye kunonea midomo ya mwingine alivyo,
ndivyo, alivyo mtu ajibuye maneno yaliyo sawa.
27Fanya kazi zako za huko nje, kajitengenezee mashamba yako,
kisha jijengee nyumba yako!
28Usiwe shahidi ya kumshinda mwenzio bure!
Je? Huko hutadanganya kwa midomo yako?
29Usiseme: Kama alivyonitendea mimi, ndivyo, nitakavyomtendea naye,
nitamlipisha kila mtu matendo yake.
30Nilipopita penye shamba la mvivu
napo penye mizabibu ya mtu aliyepotelewa na akili,
31nikapaona, pote palikuwa miiba tu,
pote palikuwa pamefunikwa na viwawi,
nacho kitalu chake cha mawe kilikuwa kimebomoka.
32Nilipoyaona nikayashika na kuyaweka moyoni mwangu mimi,
niyatumie ya kunionya.
33Ukitaka kulala bado kidogo na kupumzika bado kidogo
na kukunja mikono kitandani bado kidogo,
34kisha umaskini wako utakujia na kupiga mbio
pamoja na ukosefu ulio kama mtu aliyevaa mata.