The chat will start when you send the first message.
1Kama theluji isivyopatana na kiangazi,
kama mvua isivyopatana na mavuno,
ndivyo, macheo yasivyopatana na mpumbavu.
2Kama ndege anavyojiendea tu, kama kinega anavyoruka,
ndivyo, kiapizo cha bure kilivyo, hakimfikii aapizwaye.
3Mjeledi humpasa farasi, nayo hatamu humpasa punda;
ndivyo, fimbo inavyoipasa migongo ya wapumbavu.
4Usimjibu mpumbavu na kuufuata ujinga wake,
usije nawe mwenyewe kufanana naye!
5Tena umjibu mpumbavu na kuufuata ujinga wake,
asijiwazie mwenyewe kuwa mwerevu wa kweli!
6Mwenye kujikata miguu au mwenye kujinywesha makorofi
ni mtu apelekaye habari kwa kutuma mpumbavu.
7Kama miguu ya kiwete isivyotumika,
ndivyo, fumbo lilivyo kinywani mwa wapumbavu.
8Kama kutupa kifuko cha vito katika chungu ya mawe kulivyo,
ndivyo, kumpa mpumbavu macheo kulivyo.
9Mwiba uliochoma mkono wa mlevi
ni fumbo lililomo vinywani mwa wapumbavu.
10Fundi hutengeneza yote mwenyewe,
lakini mpumbavu atafutaye watu wa mshahara
huwapa kazi ya mshahara walio wapitaji tu.
11Kama mbwa anavyoyarudia matapiko yake,
ndivyo, mpumbavu anavyoufanya ujinga wake mara ya pili.
12Kama unaona mtu aliye mwerevu wa kweli machoni pake mwenyewe,
basi, mpumbavu hutegemeka kuliko huyo.
13Mvivu husema: Simba yuko njiani,
kweli simba yuko barabarani katikati.
14Mlango hupinduka kwa bawaba zake,
naye mvivu hujipindua kitandani pake.
15Mvivu akiutia mkono wake katika bakuli
hushindwa kuurudisha kinywani mwake.
16Mvivu ni mwerevu wa kweli machoni pake
kuliko watu saba wanaojua kujibu vizuri.
17Akamataye masikio ya mbwa apitaye
ni mtu ajitiaye katika magomvi yasiyo yake.
18Kama mwenye wazimu alivyo
atupaye mishale yenye moto ya kuua watu,
19ndivyo, alivyo mtu amdanganyaye mwenziwe,
akasema: Je? Mimi sikumchekesha tu?
20Kwa kukosa kuni moto huzimika,
vivyo kwa kukosa msingiziaji ugomvi hukoma.
21Makaa hufaa juu ya makaa yawakayo, nazo kuni hufaa motoni;
ndivyo, mtu mgomvi anavyofaa kuchochea magomvi.
22Maneno ya msingiziaji ni kama vyakula vya urembo
vinavyoshuka kuingia tumboni ndani.
23Kama fedha zenye mitapo zilizobandikwa juu ya kigae
ni midomo isemayo maneno yapendezayo sana, moyo ukiwa mbaya.
24Kwa maneno ya modomo yake mchukivu hujificha,
namo moyoni mwake umo udanganyifu, alioutia humo.
25Akisema maneno mazuri mno, usimtegemee!
Kwani moyoni mwake yamo matapisho saba.
26Uchukivu hujificha katika ujanja,
lakini shaurini ubaya wake huumbuliwa.
27Achimbaye mwina hutumbukia mwenyewe mle ndani,
naye aporomoshaye jiwe hupondwa nalo.
28Ulimi wenye uwongo huwachukia, uliowaumiza,
nacho kinywa kisemacho mororo huangamiza.