Mashangilio 47

Mashangilio 47

Mungu wa Isiraeli ni mfalme wa makabila yote.

1Makabila yote ya watu, pigeni makofi! Mwimbieni Mungu kwa shangwe na kumpigia vigelegele!

2Kwani Bwana alioko huko juu huogopesha, ni mfalme mkubwa azitawalaye nchi zote.

3Aliteka makabila ya watu, watutii, nazo koo nzima, zituangukie miguuni.

4Akatuchagulia fungu, liwe letu; ndilo, mpendwa wake Yakobo ajivunialo.[#Sh. 16:6; 5 Mose 8:7-10.]

5Mungu alipaa na kushangiliwa, Bwana ndiye aliyepigiwa baragumu.[#Sh. 68:19.]

6Mwimbieni Mungu na kupaza sauti! Mwimbieni mfalme wetu na kupaza sauti!

7Kwani aliye mfalme wa nchi zote ndiye Mungu, mwimbieni nyimbo zenye maana![#Sh. 93:1.]

8Mungu anawatawala wamizimu nao, Mungu anakaa katika kiti chenye utakatifu wake.

9Wakuu wa makabila ya watu wamekusanyika, wawe ukoo wa Mungu wa Aburahamu, kwani ngao za hapa chini ni zake Mungu, ametukuka sanasana.[#Sh. 89:19.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania