The chat will start when you send the first message.
1Mungu, wewe u Mungu wangu, ninakutafuta mapema; roho yangu ina kiu ya kunywea kwako, nazo nyama za mwili wangu zinakutunukia sana, hapa katika nchi kavu ichokeshayo kwa kuwa pasipo maji.[#1 Sam. 22:5; 23:14; 24:1; Sh. 42:3; 143:6.]
2Hivyo ndivyo, nilivyokutazamia Patakatifu pako, niione nguvu yako na utukufu wako.
3Kwani upole wako ni mwema kuliko uzima; kwa hiyo midomo yangu sharti ikusifu.
4Hivyo nitakutukuza siku zangu zote, nitakazokuwapo, Jina lako nitaliinulia mikono yangu.
5Hivi vinaishibisha roho yangu kama kiini cha mafuta, midomo yangu ikikupigia vigelegele, kinywa changu kikikushangilia.
6Ninapokwenda kulala ninakukumbuka, napo ninapoamka ninayawaza mambo yako.
7Kwani wewe ndiwe uliyenisaidia, namo kivulini mwa mabawa yako ninapiga shangwe.
8Roho yangu inagandamana nawe wewe, mkono wako wa kuume ukanishikiza.
9Lakini wao wanaoitafuta roho yangu, waiangamize, sharti washuke kuzimuni huko ndani ya nchi.
10Watu watawatoa, wauawe kwa ukali wa panga, kisha watakuwa chakula chao mbwa wa mwitu.
11Lakini mfalme atafurahia kuwa wake Mungu, wote wamwapiao yeye watashangilia, kwani vinywa vyao wasemao uwongo vitafumbwa.