Mashangilio 70

Mashangilio 70

Kuomba msaada wa Mungu.

(Taz. 40:14-17.)

1Mungu, piga mbio, uniopoe! Bwana, pigambio, unisaidie![#Sh. 38:1.]

2Sharti wapatwe na soni wakiumbuliwa walioitafuta roho yangu. Sharti warudishwe nyuma na kutwezwa wao waliopendezwa na mabaya yaliyonipata mimi.

3Sharti warudi nyuma na kuona soni wale walioniambia: Weye! Weye!

4Sharti wachangamke na kufurahiwa wote wakutafutao! Waupendao wokovu wako waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Mungu!

5Nami mnyonge, hata mkiwa; Mungu, piga mbio, unijie! Msaada wangu na wokovu wangu ndiwe wewe; wewe Bwana, usinikawilie!

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania