The chat will start when you send the first message.
1Malaika wa tano alipopiga baragumu, nikaona nyota iliyokuwa imetoka mbinguni, ikaanguka nchini. Kisha ikapewa ufunguo wa kisima cha kuzimu,[#Ufu. 9:10; 20:1.]
2ikakifungua hicho kisima cha kuzimu. Ndipo, ulipopanda moshi kutoka mle kisimani kama moshi wa jiko kubwa. Jua likatiwa giza, hata anga vilevile kwa ajili ya moshi huo wa kisimani.[#Yoe. 2:2,10.]
3Mle katika moshi mkatoka nzige, wakazifunika nchi, wakapewa nguvu, kama nge wa nchi walivyo na nguvu.
4Wakaambiwa, wasiyapotoe majani ya nchi wala cho chote kilicho kibichi, wala miti yo yote, ila wawapotoe watu tu wasio na muhuri ya Mungu mapajani.[#Ufu. 7:3.]
5Hawakupewa kuwaua, ila walipewa, wawaumize tu miezi mitano. Maumivu hayo yalikuwa kama maumivu ya nge, akimwuma mtu.
6Siku zile watu watakutafuta kufa, wasikuone; watakutunukia kufa, lakini kufa kutawakimbia.[#Luk. 23:30.]
7Umbo la nzige hao lilikuwa limefanana kama la farasi walio tayari kupiga vita. Vichwani pao hapo juu palikuwa kama vilemba vilivyofanana na dhahabu. Nyuso zao lilikuwa kama nyuso za watu.[#Yoe. 2:4.]
8Nywele, walizokuwa nazo, zilikuwa kama nywele za wanawake, nayo meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
9Vifuani walikuwa na ngao kama ngao za vyuma. Uvumi wa mabawa yao ulikuwa kama uvumi wa magari yavutwayo mbiombio na farasi wengi kwenda vitani.
10Walikuwa wenye mikia kama ya nge yenye machomeo; namo mikiani mwao ndimo, nguvu zao zilimokuwa za kuwapotoa watu miezi mitano.[#Ufu. 9:19.]
11Wana mfalme wao, ni malaika wa kuzimu, jina lake Kiebureo huitwa Abadoni, Kigiriki huitwa Apoloni.[#Ufu. 9:1.]
12Pigo la kwanza limekwisha pita; tazama, yako bado mawili, yanakuja baadaye.[#Ufu. 8:13; 11:14.]
13Malaika wa sita alipopiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe nne za meza ya Bwana ya dhahabu iliyokuwako mbele ya Mungu,[#Ufu. 8:3; 2 Mose 30:1-3.]
14ikamwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu: Wafungue wale makaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa wa Eufurati.[#Ufu. 16:12.]
15Ndipo, walipofunguliwa wale malaika wanne waliokuwa wamewekewa saa hii ya siku hii ya mwezi huu wa mwaka huu, waliue fungu la tatu la watu.[#Ufu. 8:7-12.]
16Hesabu ya vikosi vya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi (20000000); ndiyo hesabu yao, niliyoisikia.
17Nilipowatazama wale farasi nao waliowapanda, nikawaona kuwa hivyo: walikuwa wamevaa nguo za vyuma kama za moto, nyingine nyeusi, nyingine za manjano. Vichwa vya farasi vilikuwa kama vya simba, tena katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na viberitiberiti.
18Fungu la tatu la watu likauawa kwa mapigo hayo matatu, kwa moto na kwa moshi na kwa viberitiberiti vilivyotoka vinywani mwao.
19Kwani nguvu za hao farasi zimo vinywani mwao namo mikiani mwao. Kwani mikia yao imefanana na nyoka wenye vichwa; hiyo ndiyo, waliyopotoa nayo.
20Watu waliosalia, wasiouawa na mapigo hayo, hawakuyajutia matendo ya mikono yao, maana hawakuacha kutambikia mizimu na vinyago vya dhahabu na vya fedha na vya shaba na vya mawe na vya miti visivyoweza kuona wala kusikia wala kwenda.[#Ufu. 16:9,11,21; 1 Kor. 10:20.]
21Kwa hiyo hawakujutia wala uuaji wao wala uchawi wao wala ugoni wao wala wizi wao.