The chat will start when you send the first message.
1Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,[#Mwa 3:19; 47:29; Kum 31:14; 2 Sam 14:14; Ayu 30:23; 34:15; Zab 89:48; Mhu 12:7]
2Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujioneshe kuwa shujaa na hodari;[#Yos 23:14; Ebr 9:27]
3uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;[#Kum 17:19; 29:9; Yos 1:7; 1 Nya 22:12,13]
4ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.[#2 Sam 7:25; Zab 132:12; 2 Fal 20:3; 2 Sam 7:12]
5Na zaidi ya hayo, unajua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kumwaga damu wakati wa amani akilipiza kisasi cha vita, mshipi akautia damu ya vita uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.[#2 Sam 3:39; 18:5-14; 19:5-7; 3:27; 20:10]
6Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani.[#Mit 20:26]
7Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako.[#2 Sam 19:31; 9:7; 17:27]
8Hata, angalia, yuko pamoja nawe Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu, ndiye aliyenilaani kwa laana kuu siku ile nilipokwenda Mahanaimu; lakini akashuka kunilaki kule Yordani, nami nikamwapia kwa BWANA, nikamwambia, Mimi sitakuua kwa upanga.[#2 Sam 16:5]
9Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu.[#Kut 20:7; Ayu 9:28]
10Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.[#1 Fal 1:21; Ayu 14:1; Mhu 12:5; Mdo 2:29; 13:36; 2 Sam 5:7]
11Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arubaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.[#2 Sam 5:4; 1 Nya 29:26,27]
12Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana.[#1 Nya 29:23; 2 Nya 1:1]
13Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akaja kwa Bathsheba mamaye Sulemani. Naye akasema, Je! Umekuja kwa amani?[#1 Sam 16:4]
14Naye akajibu, Kwa amani. Tena akasema, Nina jambo ninalotaka kukuambia. Naye akamwambia, Sema.
15Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili mimi nimiliki; lakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa BWANA.[#1 Nya 22:9; 28:5-7; 2 Nya 20:6; Ayu 9:12; 23:13; Zab 115:3; 132:10; Mit 19:21; 21:30; Isa 14:27; 43:13; Dan 2:21; 4:25,35; Mdo 5:39]
16Basi sasa nina haja moja ninayokuomba, usinikataze hiyo. Naye akamwambia, Sema.
17Akasema, Nakusihi nena na Sulemani, mfalme (kwa kuwa hawezi kukukatalia neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami.[#1 Fal 1:3,4]
18Naye Bathsheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako.
19Basi Bathsheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kulia.[#Kut 20:12; Law 19:32; Mit 23:22; 31:28; Zab 45:9; 110:1; Mt 20:21; 25:33]
20Ndipo akasema, Haja moja ndogo nakuomba; usinikatalie. Mfalme akamwambia, Omba, mama; kwa kuwa siwezi kukukatalia neno.
21Naye akasema, Nataka Adonia, ndugu yako, aozwe Abishagi, Mshunami.
22Mfalme Sulemani akajibu, akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya.[#1 Fal 1:7]
23Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe.[#Rut 1:17; 1 Sam 14:44; 2 Sam 3:9,35; 19:13; 1 Fal 20:10; 2 Fal 6:31]
24Basi kwa hiyo, BWANA aishivyo, aliyenithibitisha na kunikalisha katika kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, akanifanyia nyumba, kama alivyoahidi, hakika atauawa leo hivi Adonia.[#2 Sam 7:11]
25Mfalme Sulemani akatuma kuwa jambo hilo liwe mkononi mwa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa.
26Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Nenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu.[#Yos 21:18; Yer 1:1; 1 Sam 23:6; 2 Sam 15:24,29; 1 Sam 22:20]
27Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa BWANA; ili alitimize neno la BWANA, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo.[#1 Sam 2:31]
28Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa BWANA, akazishika pembe za madhabahu.[#1 Fal 1:7,50; Kut 21:14; 38:2]
29Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa BWANA, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Nenda, umuue.
30Basi Benaya akaja Hemani kwa BWANA, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ila nitakufa papa hapa. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu.
31Mfalme akamwambia, Fanya alivyonena, umpige, ukamzike; ili uniondolee mimi na nyumba ya babangu damu aliyoimwaga Yoabu bure.[#Kut 21:14; Hes 35:33; Kum 19:13; 21:8,9]
32Naye BWANA atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda.[#Mwa 4:11; 9:6; Amu 9:24; Zab 7:16; 140:11; 2 Sam 3:27; 20:10; 2 Nya 21:13; Est 1:19]
33Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.[#2 Sam 3:28,29; Mit 16:7; 25:5; Isa 9:6,7; Flp 4:7; Mdo 7:45,46]
34Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani.[#Yos 15:61; Mt 3:1]
35Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari.[#Hes 25:11-13; 1 Sam 2:35; 1 Nya 6:53; 24:3]
36Tena, mfalme akatuma watu akamwita Shimei, akamwambia, Ujijengee nyumba humu Yerusalemu, ukae ndani yake, wala usitoke humo kwenda mahali popote.[#2 Sam 16:5; Mit 20:8,26; 21:3]
37Kwa kuwa siku ile ya kutoka kwako, na kuvuka kijito Kidroni, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.[#2 Sam 15:23; 2 Fal 23:6; Yn 18:1; Law 20:9; Yos 2:19; 2 Sam 1:16; Eze 18:13]
38Naye Shimei akamwambia mfalme, Neno hili ni jema; kama alivyosema bwana wangu mfalme, ndivyo atakavyofanya mtumwa wako. Basi Shimei akakaa Yerusalemu siku nyingi.
39Ikawa miaka mitatu ilipokwisha, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi, mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Wakamwambia Shimei, wakasema, Angalia, watumwa wako wako huko Gathi.[#1 Sam 27:2]
40Shimei akaondoka, akatandika punda wake, akaenda Gathi kwa Akishi, ili kuwatafuta watumwa wake. Akaenda Shimei, akawaleta watumwa wake toka Gathi.[#Mit 15:27]
41Naye Sulemani akaambiwa, ya kwamba Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi, na kurudi tena.
42Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile utakapotoka ukaenda mahali popote, ujue kwamba hakika utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?[#Zab 15:4]
43Mbona basi hukukishika kiapo chako kwa BWANA, na amri niliyokuagiza?[#Eze 17:19]
44Tena, mfalme akamwambia Shimei, Umejua uovu wote uliouona moyoni mwako, uliomtenda Daudi baba yangu; basi kwa hiyo BWANA atakurudishia uovu wako kichwani pako mwenyewe.[#Zab 7:16]
45Ila mfalme Sulemani atakuwa amebarikiwa, na kiti cha enzi cha Daudi kitathibitika mbele za BWANA hata milele.[#Mit 25:5]
46Basi mfalme akamwamuru Benaya, mwana wa Yehoyada; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Nao ufalme ukawa imara mkononi mwa Sulemani.